**************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Umoja wa makanisa ya mkoa wa Arusha(UKAMA) wameadhimisha kifo cha Yesu kwa kuhamasisha amani na mshikamao kwa watanzania wote.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Sheik Amri Abeid yamebeba jumbe mbalimbali kutoka kwa maaskofu pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta ambaye ameliomba kanisa kumuombea Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu ili Mungu aendelee kumlinda na kuweza kulitumikia Taifa kwasababu watanzania wote wanamtumaini Mungu.
Kimanta alieleza kuwa watanzania wakiwa karibu na Mungu ndipo upendo na mshikamano utakapoongezeka miongoni mwao huku akiwataka kutotilia maanani yanayoendelea katika mitandoa ya kijamii kwani nchi inaendeshwa kwa utaratibu na mfumo.
“Nchi ipo salama kwasababu kuna watu wanafanya kazi na sio kwasababu ya mitandao ya kijamii, siwaambie msiingie na kusoma yaliyomo humo bali pitieni na muyaache huko huko lakini pia muuendelee kuea wacha Mungu,”Alisema Kimanta.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini kati Askofu Dkt Solomon Massangwa alieleza kuwa ni vema wazazi na walezi wakawafundisha watoto wao mahusia mazuri kwani kwa kufanya hivyo taifa litapona na kuwa salama.
“Wakati huu tujikabidhi mikononi mwa Mungu huku tukiwafundisha watoto wetu yaliyo mema kwaajili ya amani na mshikamano wa taifa letu kwa sasa na baadae kwani kwa kufanya hivi taifa letu litashinda na kuwa salama lakini pia tufanye kazi kwa bidii na maarifa,”Alieleza.
Kwa upande wake Askofu wa jimbo kuu Katoliki Arusha, Mhashamu Baba Askofu Isaac Amani akihubiri kuhusiana na nguvu ya msalaba alisema kuwa msalaba umetumika kuwaokoa wanadamu nani utambulisho wa kukiri upendo wa Mungu.
“Msalaba utupe nguvu ya kupokea kifo na kuingia katika uzima, na pia kiwe ni chombo cha kutafakari ufiasi wetu kwa Yesu ambaye ushindi wake umetuoko dhidi ya dhambi na maovu yote,” Alisema Mhashamu Askofu Isack Amani.
Naye Mwenyekiti wa Umoja huo Dkt.Stanley Hotay ambayre pia ni Askofu wa kanisa la Anglikana ameluwataka wakristo kumuomba Mungu awasaidie katika kipindi hiki ikiwa ni pamoja na kutulia,kujiheshimu na kuhudhuria katika nyumba za ibada.
Sambamba na hayo pia Askofu Oral Sossy wa kanisa la TAG alisema kuwa ndani ya makanisa wanatengeneza hivyo serikali isiwe na wasiwasi kwa habari ya kanisa kuwa kwani amani ipo na itaendelea kudumu na kuimarika.