Home Michezo SIMBA SC YAJIPANGA KUONDOKA NA POINTI TATU DHIDI YA KLABU YA AS...

SIMBA SC YAJIPANGA KUONDOKA NA POINTI TATU DHIDI YA KLABU YA AS VITA HAPO KESHO

0

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imepania kuendeleza ushindi katika mechi ya hapo kesho dhidi ya As Vita katika hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika.

Mchezo huo utapigwa katika majira ya Saa 10 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki, Simba Sc inahitaji ushindi kwenye mechi hiyo ili iweze kujihakikishia inafuzu hatua ya robo fainali katika michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kocha msaidizi wa klabu hiyo Selemani Matola amesema timu ipo fiti kuwavaa As Vita na wanaenda kusaka alama tatu ili waweze kujihakikishia wanasonga mbele kwenye hatua inayofuata.

“Kesho ni lazima tupate matokeo ili tusonge mbele, tumejipanga kupata matokeo. Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri”. Amesema Matola.

Nae Nahodha wa klabu ya Simba John Bocco amesema wao kama wachezaji wapo vizuri kwani watafanya kila ambalo linawezekana kwa maana yale yote mwalimu ambayo amewaelekeza ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi kwenye mechi hiyo.

“Kwa upande wetu kama wachezaji tuko vizuri, tuna ari nzuri ya kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu. Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali” Amesema Bocco.