Home Mchanganyiko MHE. MCHENGERWA AWASILI KATIKA OFISI YAKE NA KUANZA KAZI BAADA YA KUAPISHWA

MHE. MCHENGERWA AWASILI KATIKA OFISI YAKE NA KUANZA KAZI BAADA YA KUAPISHWA

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisalimiana na baadhi ya watumishi wa ofisi yake alipowasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi ya Mtumba iliyopo Mji wa Serikali mara baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino Dodoma. Walioambatana nae ni Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake mara baada ya kuapishwa na kuwasili ofisini hapo ili kuanza kazi rasmi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Nbumbaro (kulia) mara baada ya kuapishwa na kuwasili katika ofisi yake iliyopo Mtumba kwenye Mji wa Serikali.