…………………………………………………………………………….
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ,amemtaka Waziri w Fedha Dk.Mwigulu Nchemba kutanua wigo wa ukusanyaji kodi akiwataka kuacha kutumia nguvu kubwa na badala yake akili na maarifa na kuacha kuchukua fedha na vifaa vyao vya kazi pamoja na kufunga akaunti zao mnau biashara.
Maagizo hayo ameyatoa leo April 1,2021 Ikulu Chamwino, Dodoma wakati akimuapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga ,Mawaziri pamoja na Manaibu waliteuliwa jana na Rais.
Rais Samia amesema kuwa zimekuwa zikitumika nguvu kubwa kukusanya mapato ya Serikali zimekuwa zikisababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kwenda kufungua katika nchi nyingine na kusababisha Serikali inakosa mapato.
Amesema kuwa nimemsikia Makamu wa Rais wakati anazungumzia amesma Serikali kuongeza ukusanyaji mapato kwa mwezi kufikia Sh.Trilioni mbili ambapo amesema hilo linawezekana lakini ametoa angalizo kuwa akili na maarifa ndio inatakiwa kutumika kuongeza ukusanyaji huo wa mapato ya Serikali.
Amewambia Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba lazima wasimamie ukusanyaji mapato vizuri, hakuna sababu ya kutumia nguvu katika kukusanya kodi na Nguvu kubwa sana inatumika na badala ya kusaidia wafanyabiashara mnasababisha wafunge biashara hivyo tumieni weledi na maarifa katika ukusanyaji wa kodi.” amesisitiza
Hata hivyo Rais Samia amewakumbusha mawaziri wote kuwa serikali ni moja wafanye kazi kwa ushirikiano na hatosita kumuondoa yeyote ambaye atainua mabega yake akiwataka kwenda kwa watanzania kutatua changamoto zao.
Pia Rais Samia amesema kuwa upo uwezekano kuwaapisha viongozi wengine Jumanne wiki ijayo baada ya sikukuu ya Pasaka kumalizika