Home Mchanganyiko WAZIRI NDALICHAKO AKABIDHI MAGARI 38 KWA WATHIBITI UBORA WA SHULE ZA KANDA...

WAZIRI NDALICHAKO AKABIDHI MAGARI 38 KWA WATHIBITI UBORA WA SHULE ZA KANDA NA WILAYA

0

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza na watumishi wa wizara hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Moshi Kabengwe,akieleze mikakati wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

 

Baadhi ya Watumishi wakifatilia Hotuba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya Magari yaliyotolewa  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

 

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akikata utepe kuashiria ugawaji wa  Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiingia kwenye gari mara baada ya kukabidhi Magari 38  kwa wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiwa ndani ya gari akienda mara baada ya kuwakabidhi Magari 38  wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akimkabidhi ufunguo wa gari Mthibiti Mkuu ubora wa Shule Kanda ya Ziwa Bw.Victor Bwindiki  mara baada ya kuwakabidhi  Magari 38  wathibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiwa na Naibu wake Mhe Omary Kipanga wakimsikiliza Mthibiti Mkuu ubora wa Shule Kanda ya Ziwa Bw.Victor Bwindiki wakati akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Kukabidhi Magari 38 kwa Wathibiti Ubora wa Shule za Kanda na Wilaya hafla iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako  amegawa magari 38 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6  kwa Wathibiti Ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya kwa lengo la kuimarisha shughuli za uthibiti ubora wa shule nchini.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 31,2021 Jijini Dodoma Prof.Ndalichako ,amesema suala la usafiri ni la muhimu katika kuwawezesha Wathibiti ubora wa shule kuzifikia shule na vyuo vya ualimu kwa wakati ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Wizara yangu ina jukumu la kusimamia mfumo wa uthibiti ubora wa shule na kufanya tathmini ya ujifunzaji na ufundishaji katika shule na vyuo vya ualimu na kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma ili kuinua ubora wa Elimu nchini, hivyo magari haya yatarahisisha na kuwezesha majukumu haya kufanyika kwa ufanisi na weledi,” amesema Waziri Ndalichako.
Hata hivyo Prof. Ndalichako  ametoa agizo kwa Wathibiti Ubora wa Shule wa Wilaya kuanza mara moja kukagua shule za sekondari badala ya kukagua shule za msingi pekee. 
Waziri Ndalichako amesema  kuwa haileti maana yoyote kwa Mthibiti Ubora wa shule wa Wilaya kukagua shule za msingi pekee huku akiwa na sifa na mafunzo yanayomwezesha kukagua pia shule za sekondari.
Waziri Ndalichako amesisitiza kwamba agizo hilo linalenga kuimarisha  matumizi mazuri ya fedha kwa kupunguza safari ambapo ukaguzi wa eneo moja umekuwa ukifanywa na  Wathibiti ubora wawili tofauti wenye sifa na mafunzo yanayolingana.
Awali akizungumza kwa niaba ya Wathibiti Ubora wa Shule, Victor Bwindiki ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Ziwa ameishukuru Serikali kwa jinsi inavyoendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuahidi kuendelea kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kwa Walimu, Wakufunzi na Viongozi wa elimu ili kuinua ubora wa elimu nchini.
Magari yaliyotolewa yatapelekwa katika ofisi  10 za Kanda, 27 Ofisi za Halmashauri na moja litabaki Wizarani.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary
Kipanga amewataka wathibiti Ubora wa shule kuyatumia magari hayo kwa
malengo yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.