Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, hivi karibuni, aKIweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Kijiji cha Chimate, utakaohudumia Wananchi zaidi ya 2798 Wilayani Nyasa ambao umejengwa na Serikali na utagharimu tsh 390,87,000 hadi kukamilika kwake .Mradi huu umetatua tatizo la maji katika kijiji hicho kwa kuwa awali hapakuwa na mradi wa maji.
***********************************
Na Steven Augustino, Nyasa
SERIKALI Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma imeupongeza Waakara wa maji Mijini na Vijijini Ruwasa Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Nyasa kwa ujenzi wa Mradi Mzuri ambao na kwamba kukamirika kwake kutasaidia ukamirishaji wa juhudi za Serika za kumtua mama ndoo kichwani.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba muda mfupi baada ya kukagua na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Mradi huo uliojengwa na wakara huo katika Kijiji cha Chimate ambao umepaangwa kuhudumia zaidi ya Wananchi 2,798 wa kijiji hicho baada ya kukamirika kwake.
Aidha Dc ,Chilumba pamoja na mambo mengine alidai kuridhishwa na Ufanisi wa mradi huo kwa kuwa, Mpaka anaweka jiwe la Msingi Mradi huo umeanza kutoa huduma kwa Wananchi na akatumia nafasi hiyo kuwataka waendeleze juhudi hizo na kuhakikisha wanamaliza Kero ya ukosefu wa maji Wilayani humo.
Kufuatia hali hiyo pia Dc, Chilumba akatumiaa nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Chimate kuitunza Miundombinu ya Maji ili iweze kuwanufaisha katika kipindi cha miaka mingi enda hata haribu vyanzo vya maji.
Awali Akitoa Taarifa fupi ya Mradi wa maji kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhandisi Jeremia Maduhu amesema Ruwasa Nyasa Imetekeleza mradi huo kwa njia ya Force account na kufanikiwa, kutekeleza mradi huo kwa kuwa mpaka sasa umefikia asilimia 85 na unatarajia kukamilika April 15 mwaka huu.
Amezitaja kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa Temki jipya, lenye ujazo wa lita 75,000, Ujenzi wa Vituo vya kuchotea maji 18, na Tayari vituo 10 vimeshaanza kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi na ujenzi wa mtandao wa bomba za kusambazia maji kilometa 18.53, kazi ambayo imefanyika na iliyobaki ni kuunganisha ili vituo nane vilivyobabi viweze kutoa huduma ya maji kwa Wananchi wa Kijiji cha Chimate Wilayani Nyasa.
Alisema kwa sasa ujenzi wa Mradi huo umefikia asilimia 85 ya ukamilishaji wake, na Vituo kumi vya maji vimeshaanza kutoa maji na wananchi wananufaika na huduma ya maji safi na salama, na mpaka kukamilika kwake, Mradi unatarajia kugharimu milioni 390,870,000 Fedha ambazo zimetolewa na Serikali kupitia Mradi wa EP4R.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha chimate Waliipongeza Serikali kwa Kuwajengea Mradi huo ambao umetatua kero ya Maji katika Kijiji hicho kwa Kuwa awali hapakuwa na Huduma ya Maji safi, hali ambayo iliwalazimu kutembea umbali wa takribani kilometa 5 hadi 10 kufuata maji,katika Vyanzo vya asili.