Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango,akiapa kuwa Makamu wa Rais mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahimu Juma,uapisho umefanyika Ikulu Chamwino na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo leo Ikulu, Chamwino Dodoma.
………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameapishwa lhuku akiwahakikishia watanzania kukidhi matamanio yao Katika maendeleo na kuwa atakuwa mtiifu kwa Rais, Wabunge na chama chake (CCM) bila kuleta usaliti kwa sababu ya fedha kama ambavyo Yuda Eskarioti alivyofanya kwa Yesu Kristo.
Dk. Mpango amesema hayo leo Machi 31,202 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma wakati akila kiapo cha utumishi katika nafasi yake mpya ya Makamu wa Rais huku akisema kuwa hakutegemea kuwa yeye mtoto wa maskini kutoka Buhigwe angeweza kuteuliwa kuitumikia nafasi hiyo.
“Nitakuwa msaidizi mwaminifu na mzalendo kwa nchi yangu, sitakuwa kama Yuda, nitatekeleza kwa bidii na weledi kazi zote utakazonilekeza, nitatekeleza majukumu hayo chini ya uongozi na utumishi wako. nitume hata usiku na Mchana nikachape kazi,” amesisitiza.
Hata hivyo amesisitiza kuwa atashirikiana na viongozi wengine bega kwa bega ili kuleta maendeleo kwa watanzania .
“Naishuku Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupitisha jina langu na wabunge walinipitisha kwa kura zote, Bunge letu tukufu limekuwa hazina kubwa kwangu kwani nimevuna mengi katika kipindi chote nilichokuwa ndani ya bunge,”alisema na kuongeza;.
“Nawashukuru wananchi wa Buhigwe Kigoma kwa kuniamini na kunipigia kura za kishindo, nawaomba watanzania muendelee kuniombea niweze kukidhi matarajio yao na niwe mnyenyekevu, mtii na nitakayesimamia maslahi ya wananchi wanyonge,” amesema
.