*****************************************
Machi 2021: Bolt, kampuni inayoongoza kwa huduma za usafiri barani Afrika imezindua huduma ya Bolt Web App, njia nyingine rahisi na nafuu ya kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao.
Bolt Web App ni suluhisho sahihi kwa wanaomiliki simu za kawaida ambazo mara nyingi zina uwezo mdogo wa kimatumizi, kuhifadhi taarifa na wa kuunganishwa na huduma za mtandao. Mara nyingi watumiaji wa simu za aina hii pia wanajali gharama za matumizi ya data. Mfumo huu mpya wa Bolt Web App pia unaweza kutumiwa na wale wanaohitaji kuomba usafiri kupitia kompyuta zao.
Remmy Eseka, Meneja wa Bolt Tanzania alisema,” Hapa Bolt daima tunafanya kazi kuhakikisha kuwa usafiri unapatikana kwa urahisi katika maeneo ya mjini. Bolt Web App inawawezesha wateja ambao hawatumii simu za kisasa (smartphones) na wale wanaoishi katika maeneo ambapo huduma za mtandao wa intaneti ni ghali ama ngumu kupatikana kupata usafiri wa uhakika kwa bei nafuu. Bolt inajitahidi kuwahakikishia wateja kuwa wanaweza kupata usafiri wa Bolt haraka popote walipo, bila kujali aina ya simu au mfumo wa mawasiliano wanaotumia. Kupitia njia hii, watumiaji wana mbinu mbadala ya kuagiza na kupata usafiri wa uhakika.”
Bolt Web App inapatikana kwa kuingiza namba ya simu na kutumiwa namba ya OTP kwenye simu ya mtumiaji. Mara uthibitisho unapotolewa, mteja anaweza kuchagua sehemu anayotaka kwenda.
Usafiri kupitia Bolt Web App unalipiwa kwa njia ya pesa taslim pekee. Wateja wanaweza kutoa taarifa kuhusu ubora wa safari yao na dereva husika. Pia Bolt Web App inakuwezesha kupata usafiri wa aina mbali mbali ikiwemo Bolt, Bolt Boda, Bolt Bajaji na Bolt XL, ambapo mteja anaruhusiwa kuchagua aina ya usafiri anaotaka.
Uzinduzi wa Web App unahakikisha kuwa Bolt Web App sasa ipo mkononi mwa watumiaji wa Dar es Salaam, Arusha na Mwanza nchini Tanzania, pamoja na nchi za Afrika ya Kusini, Nigeria, Ghana na Kenya.
MWISHO
Kuhusu Bolt
Bolt ni mfumo unaoongoza wa usafiri unaolenga kufanya usafiri maeneo ya mjini kuwa rahisi, na wa uhakika kwa gharama nafuu.
Bolt ina watumiaji zaidi ya milioni 30 katika nchi 35 za Afrika na Ulaya. Huduma zake zinajumuisha kuagiza usafiri wa magari na pikipiki, pamoja na huduma za kusafirisha mizigo na chakula.