Home Mchanganyiko BUNGE LAMTHIBITISHA DK.MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS KWA 100%

BUNGE LAMTHIBITISHA DK.MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS KWA 100%

0

 

Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango  akiwashukuru wabunge waliomchagua kwa kishindo wakati wa Bunge la 12 Jijini Dodoma leo Machi 30,2021.

…………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja leo Machi 30 ,2021 limemthibitisha Dk.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Matokeo hayo yametangwa na Spika wa bunge Job Ndugai ,amesema kuwa jumla ya kura 363 zilizopigwa na zote zimethibitisha ndio.

“Naomba  kutangazia Bunge hili na nchi yetu kwa ujumla kuwa kura za hapana hakuna hata moja, kura zote 363 ni kura za ndiyo kwa hiyo amepata asilimia 100 ya kura zote.”