Home Michezo WACHEZAJI WA KMC FC WAREJEA KAMBINI,KUANZA MAZOEZI KESHO

WACHEZAJI WA KMC FC WAREJEA KAMBINI,KUANZA MAZOEZI KESHO

0

………………………………………………………………………

Kikosi cha KMC FC kimewasili kambini tayari kwa kuanza maandalizi ya michezo ya ligi kuu Soka Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho ikiwa ni baada ya kuwepo kwenye mapumziko mafupi ya kupisha michezo ya kirafiki ya kimataifa pamoja na mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Libya.

Kikosi hicho cha wana Kino Boys kimewasili jana jioni na kwamba kesho kitaanza kufanya mazoezi rasmi ili kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara pamoja na michezo ya kombe la Shirikisho ASFC.

Itakumbukwa kuwa KMC ilikuwa kwenye mapumziko kuanzia Machi 11 ambapo uongozi ulitoa siku nane na kwamba wachezaji walipaswa kurejea kambini machi 20 na kwamba kutokana na kuwepo kwa msiba wa kitaifa wa hayati Dk. John Joseph Pombe Magufuli tuliongeza siku za mapumziko hadi pale tulipo mpumzisha kiongozi wetu Machi 26 na hivyo Timu kurejea jana.

KMC FC hadi sasa ipo katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 35 ambapo katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kwenda kwenye mapumziko mafupi ilikutana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri.