Home Mchanganyiko SERIKALI YATANGAZA KUANZA KWA TAHASUSI MPYA TANO KWA AJILI YA WANAFUNZI ...

SERIKALI YATANGAZA KUANZA KWA TAHASUSI MPYA TANO KWA AJILI YA WANAFUNZI WANAOINGIA KIDATO CHA TANO MWAKA HUU

0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 29,2021 jijini Dodoma wakati akitangaza kuanza kwa tahsusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato Cha tano mwaka huu.
……………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo,ametangaza  kuanza kwa tahsusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato Cha tano mwaka huu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini.
Tahsusi hizo ni Physics,Mathematics na Computer Studies (PMC),Kiswahili, French ,Chinese (KFC),Kiswahili,English ,Chinese (KEC),Physical education,biology ,Fine art (PBF) na Physical education, geography ,economics (PGE).
Hayo ameyasema leo Machi 29,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Waziri Jafo, amesema kuwa tahsusi ya PMC itatolewa katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya  Dodoma na Shule ya Sekondari ya wavulana ya Iyunga.
Waziri Jafo amesema kuwa tahsusi ya  KFC na KEC itatolewa katika Shule ya Sekondari ya wasichana Morogoro na ya wavulana Usagara na tahsusi ya PBF na PGE  itatolewa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Makambako, Shule ya Sekondari ya wavulana Kibiti na Sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.
“Nchi yetu ilikosa kuwa na wataalam wa Michezo kutokana na kutokuwepo na tahsusi maalum,hivyo hili ni jambo jipya ambalo mwanzo halikuwepo,”amesema Jafo
Hata hivyo Mhe.Jafo ametangaza ratiba ya kubadili inaanza Machi 29 hadi April 11,2021 ambapo wanafunzi wataingia kwenye mtandao na kutumia namba zao za mitihani ya 2020 kisha mfumo utawaelekeza kwa hatua zote.
Mhe.Jafo amesema kuwa kwasasa wanafunzi hao wanafahamu walivyofaulu na kwasababu hiyo watachagua tahasusi au fani za kusomea kwa uhakika sawa na viwango vyao vya ufaulu.
Mhe.Jafo amesema kuwa  katika kipindi hicho, wanafunzi wataingia kwenye mtandao na kutumia namba zao za mitihani ya 2020 kisha mfumo utawaelekeza kwa hatua zote.
Aidha Jafo ametoa wito kwa wanafunzi kuanza leo kuingia mtandaoni kwa ajili ya kubadili Tahasusi zao mara baada ya  muda huo,kuisha April 11,2021 saa sita usiku hakutakuwa na nafasi ya kufanya uchaguzi mwingine, isipokuwa taarifa za awali ndizo zitakazotumika.