Diwani wa kata ya Sekei wa halmashauri ya jiji la Arusha Gerald John Sebastian akisaini kitabu cha maombolezo
………………………………………………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, LABDA ARUSHA.
Diwani wa kata ya Sekei wa halmashauri ya jiji la Arusha Gerald John Sebastian amesema kuwa wananchi, wafanyakazi na viongozi wote kwa ujumla wanapaswa kuishi katika mfumo ambao Hayati Rais Dkt John Magufuli ameuacha kwani umeleta nidhamu katika kila sekta.
Diwani Sebastian aliyasema hayo wakati alipokuwa akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa pamoja mapinduzi makubwa ya kimaendeleo aliyoyafanya Hayati Rais Dkt Magufuli lakini pia ameleta nidhamu makazini.
“Hayati Rais Dkt Magufuli pamoja na kutuongoza lakini pia amelikiwa mwalimu wetu, tuapaswa kiyaishi yale yote aliyofundisha, ametufanya watanzania tuheshimike na kuthaminiwa ndani na nje ya nchi yetu,” Alisema Sebastian.
Alieleza kuwa tangu amezaliwa hakujua maisha nini lakini katika uongozi wa Hayati Rais Dkt Magufuli wa miaka mitano na miezi mitano kuna mambo mengi amejifumza moja wapo ikiwa ni kujiamini na kuona kila jambo la katika hii dunia ukiwa na uhai linawezekana.
Alifafanua kuwa wakirudi nyuma miaka mitano iliyopita mikoa mingi kiuchumi, miundo mbinu na huduma za kijamii ilikuwa nyuma lakini hivi sasa mambo yamebadilika uchumi uko juu, barabara zimejengwa na kuendelea.
“Amefanya uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja umeimarika, uelewa wa haki umekuwa na kufanya kila mtu aheshimike kiukweli tunasikitika lakini tunamshukuru Mumngu kwani alitupa kiongozi mwenye maono makubwa na nchi yake na hata aliyechukua mmafasi yake ni mwanafuzi nambari moja aliyekuwa akionna, akisikiliza na kujifunza mengi kutoka kwake,”Alieleza Sebastian.
Aliwataka watanzania kutokuwa wasiwasi na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa kama alivyofanya katika bunge la katiba na kufanya kazi na Hayati Rais Magufuli kwa miaka mitano amekuwa mwanafunzi na kiranja namba moja kumsikiliza na kumuelewa hivyo wawe na imani kubwa na yeye.