Home Mchanganyiko MCHAKATO WA WILAYA CHATO KUWA MKOA HUFANYIKE-RAIS MHE.SAMIA SULUHU

MCHAKATO WA WILAYA CHATO KUWA MKOA HUFANYIKE-RAIS MHE.SAMIA SULUHU

0

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO, CHATO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewaagiza wahusika wanaotokeleza mchakato wa Wilaya ya Chato kuwa Mkoa wamalize mchakato huo.

Akizungumza katika tukio la mazishi ya Hayati John Pombe Magufuli wilayani Chato amesema wahusika wanaotekeleza mchakato huo wamalize katika ngazi zote na wapeleke Serikalini ili waangalie vigezo kama vinakidhi basi hawana budi kuruhusu.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amesema ametekeleza maagizo ya Mhe.Rais Samia Suluhu kwamba kutokana na mama mzazi wa Hayati Rais Magufuli kuwa mgonjwa, madaktari waliokuwa wakimhudumia kipindi cha nyuma wataendelea kumpa huduma kama kawaida hadi afya yake itakapotengemaa.

Nae Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi amesema kwa kipindi cha miaka mitano, nchi imepiga hatua kubwa hata kuushangaza ulimwengu kwa namna Hayati Magufuli alivyoitetea nchi kwa maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa barabara, ujenzi wa masoko makubwa nchini, huduma za usafiri wa ndege na mengine mengi.

” Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,Rais Magufuli ameondoka, ametuachia mwingine ambaye ni wewe uliyekuwa msaidizi wake wa karibu sana, tuba imani kazi unaiweza, nilifurahi sana siku ile ulipotwambia ‘Huyi aliyesimama hapa ni Rais’ tunakuamini”. Amesema Mhe.Mwinyi.

Hata hivyo kwa upande wake Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Awamu ya Saba, Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein amesema kuwa Rais John Pombe Magufuli kati ya sifa kubwa aliyokuwa nayo ni ukweli wake ulimfanya asimwogope binadamu mwenzie ila mwenyezi mungu pekee.

“Katika muungano alinitia moyo sana hasa baada ya matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu, aliniambia usifuate hayo we chapa kazi watu wataona wenyewe, na mimi nilifanya hivyo na kuufuata ushauri wake ilinisaidia”. Amesema Mhe.Dkt.Shein.