Home Mchanganyiko JENERALI MABEYO: HAYATI DKT.MAGUFULI ALIVIPENDA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

JENERALI MABEYO: HAYATI DKT.MAGUFULI ALIVIPENDA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

0

Hayati Dkt.John Magufuli alionesha kuviamini na kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama kwani alihakikisha anaviwezesha kwa mahitaji ya utendaji na kiutawala ili viweze kutekeleza majukumu yake.

Ameyasema hayo leo Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo katika tukio la kuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli wilayani Chato.

Akizungumza katika tukio hilo Mabeyo amesema Hayati Magufuli upendo wake aliuonesha kwa namna ambavyo alivishirikisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya nchini.

“Vyombo vyetu vimeshirikishwa katika shughuli zote za kiuchumi mifano michache ni ushiriki wetu wa kuulinda mgodi wa Tanzanite, kabla ya kuulinda lakini tulijenga ukuta kuzunguka mgodi huo”. Amesema Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.