Home Mchanganyiko TUENDELEE KUSHIKAMANA KULIJENGA TAIFA LETU-MHE.HEMED SULEIMAN

TUENDELEE KUSHIKAMANA KULIJENGA TAIFA LETU-MHE.HEMED SULEIMAN

0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulah akizungumza na wananchi wakati wa tukio la kuaga mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa Magufuli , Chato, Mkoani Geita Machi 25, 2021 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa Magufuli , Chato, Mkoani Geita ili kutoa nafasi kwa wananchi na viongozi mbalimbali kuaga, Machi 25, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*******************************************

NA EMMANUEL MBATILO, CHATO

Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ametuonesha njia hasa kwa kuliacha Taifa likiwa Salama hivyo tuendelee kushikamana kwa pamoja na kuendelea kulijenga Taifa.

Ameyasema hayo leo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulah wakati wa tukio la kuaga mwili wa Hayati John Pombe Magufuli wilayani Chato mkoani Geita.

akizungumza katika tukio hilo amewataka watanzania kuendelea kushirikiana kwa pamoja kulinda amani kwa taifa na kuendeleza juhudi zilizokuwa zinafanywa na Hayati John Pombe Magufuli katika kuhakikisha nchi inakuwa na amani.

“Kupitia fursa hii niendelee kuwaomba Watanzania, tuendelee kushikamana sana katika kulijenga Taifa, tayari mpendwa wetu Hayati Magufuli ametuonyesha njia, ameliacha Taifa hili likiwa salama na heshima kubwa sana, alitutoa kwenye uchumi wa chini na kutuweka kwenye uchumi wa kati”. Amesema Mhe.Suleiman.

Aidha amesema wataendelea kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu ili tuweze kulijenga Taifa bora la Tanzania.

“Rais wetu mama yetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ametuhakikishia hapataharibika kitu tuendelee kumpa mashirikiano, tuendelee kumshauri vyema, tuendelee kujitolea kwa ajili ya taifa letu, ili tuweze kulijenga taifa bora la Tanzania ambalo limepata heshima kubwa”. Amesema Mhe.Suleiman