Wananchi wa Kirumba, Ghana, Kiloleli, Nyasaka, Buzuluga, Mabatini, Mwanza mjini, Igogo, Mkuyuni, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa na Usagara wakiwa wamesimama barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza mara baada ya kuagwa katika uwanja wa CCM Kirumba leo tarehe 24 Machi 2021.