Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulah wakati wakipokea mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa Abeid Amani Karume, Zanzibar Machi 23, 2021 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa Abeid Amani Karume, Zanzibar Machi 23, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa Abeid Amani Karume, Zanzibar Machi 23, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukiwasili kwenye uwanja wa Amani kwa ajili ya tukio la kuagwa na wananchi wa Zanzibar Machi 23, 2021. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Zanzibar wakati wa tukio la kuaga mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa Amani, Zanzibar Machi 23, 2021. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
**********************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Zaidi ya watu Bilioni 3.9 Duniani wamefuatilia tukio la kumuaga Hayati John Pombe Magufuli jana Dodoma ambako tukio hilo lilikuwa la kitaifa mkoani humo.
Ameyasema hayo leo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa alipokuwa anawahutubia wananchi katika tukio la kuaga mwili wa Hayati John Pombe Magufuli visiwani Zanzibar.
“Kwa taarifa tulizonazo mpaka jana jioni zaidi ya Watu Bilioni 3.9 karibu Watu Bilioni 4 Duniani walikuwa wanafuatilia tukio la kumuaga Hayati Magufuli Kitaifa jana Dodoma na naamini leo pia itakuwa hivyo”. Amesema Mhe. Majaliwa
Aidha Waziri mkuu amesema wataendelea kutekeleza ilani kwa kukamilisha yale aliyayaanzisha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli pindi alipokuwa hai.
“Kwa niaba ya Kamati ya Mazishi Kitaifa bado tuko kwenye siku za huzuni tangu siku tumetangaziwa kifo cha Rais wetu mpendwa, ni tukio lisilo la kawaida sana kuondokewa na Rais akiwa madarakani, ila ni mipango ya Mungu na sisi viongozi tunaahidi kuendeleza Ilani na kutekeleza na kukamilisha yale aliyoyaanzisha”. Amesema Mhe.Majaliwa.
Amesema kwa kutambua upendo wa watanzania ndio maana ratiba ya kuaga imehusisha sehemu mbalimbali hapa nchini, kesho mwili utatoka hapa Zanzibar asubuhi kwa ndege maalum kuelekea mkoani Mwanza, baada ya shughuli za kuaga mkoani Mwanza, tunatarajia mwili kusafirishwa kwa gari hadi nyumbani kwake Chato, hii ikiwa ni fursa kwa watanzania kuweza kuaga katika vituo mbalimbali njiani