Home Mchanganyiko MWILI WA MAGUFULI KULALA IKULU ZANZIBAR

MWILI WA MAGUFULI KULALA IKULU ZANZIBAR

0

……………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kuwa Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli utalala  Katika Hospitali ya Jeshi Bububu hadi kesho asubuhi mwili utaondoka kwa ndege maalum kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya wakazi wa kanda ya ziwa ili nao kupata nafasi ya kuaga.

Majaliwa ameyasema hayo leo Machi 23,2021 visiwani Zanzibar wakati wa shughuli ya kumuaga Hayati Dkt.John Magufuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar 

Pia Waziri Mkuu amesema kuwa tuendelee kutoa pole kwa mke wa marehemu ambaye hakumudu kufika, leo tulimuomba kwa kweli apumzike kwa sababu kuanzia jana ana huzuni sana kwahiyo tukamsihi atangulie Mwanza tutamkuta huko.

“Mpaka jana jioni tunazo taarifa watu waliofuatilia tukio la kuaga kitaifa jana Dodoma mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli ni watu karibu bilioni 4 walikuwa wanafuatilia tukio la kuaga kwa mpendwa wetu”

“”Leo mtapata fursa ya kupita mmoja mmoja mbele ya jeneza na kumuaga, tunaamini kwa idadi hii haiwezi kutuchukua masaa mengi lakini tutakuwa hapa hata kama tutamaliza saa sita usiku, ili mradi kila mmoja anamaliza kiu ya kumuaga Kiongozi wetu””amesema Majaliwa 

Aidha Majaliwa amesema kuwa Kesho asubuhi mwili utaondoka kwenda jijini Mwanza mara baada ya kuagwa mwili  utatembea kwa gari kupita daraja la Busisi na kisha kusimama kwa dakika 10 nyumbani kwa wazazi wa mke wa marehemu.