………………………………………………………………………….
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametaja mambo matatu ambayo alielezwa na Hayati John Magufuli ni pamoja na kusimamia Maadili,Rushwa na Ubadirifu na kuitangaza Lugha ya Kiswahili.
Ramahosa ameyasema leo Machi 22,2021 jijini Dodoma katika hafla ya kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt. Magufuli uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Aidha Mhe.Ramaphosa amesema kuwa alimweleza umuhimu wa Lugha ya kiswahili kuanza kufundishwa nchini Afrika Kusini ili Afrika yote ijue lugha hiyo.
Mhe.Ramaphosa amesema kuwa Magufuli alikuwa Kiongozi mahiri wa kizazi kipya aliyesimama na kusema kiongozi anapaswa kutumikia Taifa lake na si kujinufaisha binafsi.
“Napenda kumshukuru kwa ajili ya shabaha yake na ukombozi kwa bara lote la Afrika, aliamini kuwa tunapaswa kulinda utamaduni, mila na desturi zetu pia tunapaswa kuheshimu lugha zetu.”
Hata hivyo amesema kuwa Dkt.Magufuli alikuwa ni mwinjilisti wa kila Mwafrika barani Afrika aweze kuzungumza Kiswahili, alipotembelea Afrika Kusini aliniletea boksi lililojaa vitabu vya Kiswahili akaniambia atanifundisha Kiswahili lakini ameondoka kabla hajanifundisha Kiswahili kizuri ambacho ningeweza kukizungumza hapa leo.
Hafla ya kumuaga Hayati Dkt.John Magufuli kitaifa imefanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassana pamoja na Marais wa nchi zaidi ya 10 na viongozi mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wamehudhuria tukio la kutoa heshima za mwisho.