Nabii mkuu Tanzania wa kanisa la ngurumo ya upako Dr. Geordavie kisambale akiongea katika ibada ya jumapili uliofanyika leo katika hema la kukutania la chuo cha manabii kisongo, mkoani Arusha
Bilionea wa madini aina ya Ruby kutoka Kijiji Cha Mundarara Wilayani Longido mkoani Arusha Gabriel Sendeu Laizer akisaini kitabu Cha maombolezo jana ya aliekuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Magufuli kilichopo Katika viwanja vya ofisi za mkuu wa mkoa wa Arusha (picha na Woinde Shizza , ARUSHA). Waombolezaji wakiendelea kusaini kitabu Cha maombolezo Katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
********************************************
Na Woinde shizza, ARUSHA
Watanzania wametakiwa kujitia nguvu na kuvaa ujasiri haswa katika kipindi hichi tulichopo kwenye maombolezo ya kifo cha aliekuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Magufuli ili nchi yetu iendelee kusonga mbele kimaendeleo.
Hayo yamebainishwa na nabii mkuu wa kanisa la ngurumo ya upako Dr. Geordavie kisambale alipokuwa akiongea katika ibada ya jumapili uliofanyika katika hema la kukutania la chuo cha manabii kisongo, mkoani Arusha ambapo alisema nchi yetu ipo kwenye msiba mkubwa ,ambao unamgusa kila mtanzania hivyo badala ya kuhuzunika ni lazima tujitie moyo na kuendeleza kusonga mbele
Alisema kuwa hayati Rais Magufuli
aliwatengenezea watanzania njia mahali pasipo kuwana njia bila kujali mbele kunanini,
aliwavusha watanzania bila kujali atakufa wala nini bali alijipanga kuwatengenezea watanzania njia nguvu ya kiuchumi na alitaka kuwafikisha wananchi wake Katika safari ya kuelekea kwenye kisiwa chenye azina, ambayo bila kutumia nguvu ni ngumu kufika.
Aliwataka watanzania wajue faraja inatoka kwa Mungu hivyo wasimame imara na waendelee kusonga mbele.
“Unaweza kuwa tajiri kama utajiri wako aujaweza kuvusha maskini au kuwagusa wewe ni maskini bado, Magufuli aliwekeza kwenye mioyo ya watu ,hususa ni maskini hivyo ni vyema matajiri ,viongozi waige moyo wa Rais , kupitia mafundisho yake kwa viongozi wake wote waliokuwa chini yake kuna mtu aliechukuwa roho,na huyo ndie anaitwa mwana wa Magufuli ,atakuja kuwa na roho ya magufuli na itazidi roho ya Magufuli ,na mtu huyu atatokea katika watu aliewakimbiza ,aliewaongoza atatoka mwenye roho yake atakuja kuwaletea watanzania furaha na amani”alibainisha Geordavie
Aliongeza kuwa ni vyema kila mwananchi akajifunza kuwekeza kwenye mioyo ya watu maana watu wataongea kwa niaba yao hatakama hawapo duniani watazungumza,pia aliongeza kuwa ni vyema kabla ujafikia mafanikio kujifunza kumcha Mungu na kumtegemea Mungu na sio mizungu.
Alisema kuwa nijambo moja kuwa kiongozi ,nijambo lingine kuwa kiongozi ambaye anawapenda wananchi wake na kutenda jambo ambalo litaonekana kwa wananchi ,alisema Rais Magufuli alipewa Ilani yenye vitu vingi ambayo alivisimamia pia akavitenda matendo yake yakaonekana
“Kwa swala la ugonjwa wa covid 19 nikwambie tu msikubali hofu iwatawale kisa tu mtu aliekuwa anasisitiza tusiwe na hofu ameondoka bali tuendelee kumuamini Mungu , hofu iliojaa katikati ya watu ,kama kweli watu wangekuwa wanakufa hivyo kweli Tanzania tungekuwa tumeisha kama tupo milioni 60 alafu wakafa 100 sio mbaya maana kwajinsi watu wanavyosema na kuwatia watu hofu kuhusiana na ugonjwa huu kama sio kuondolewa hofu tangu mtu wa kwanza alivyotangazwa kuwa na COVID19 hapa Tanzania adi Sasa Kama maneno yanayosewa ni yakweli ungekuta watu wote tungeshakufa au tungebaki ata milioni atufiki “Alisema Geordavie
Aliwataka wananchi kupuuza mambo ambayo yanayopandikizwa kuleta hofu zaidi kuliko ukweli halisi na kusema ni vyema tuchukue tahadhari zaidi zinazotolewa na wataalam wa afya ,huku akiwasisitiza kutochanganywa na hofu maana hofu ni adui wa maisha yako.