Home Mchanganyiko Siku ya Uchakataji Duniani (Global Recycling Day) inahitaji ushirikiano wa pamoja kwa...

Siku ya Uchakataji Duniani (Global Recycling Day) inahitaji ushirikiano wa pamoja kwa ‘Ulimwengu bila Taka’

0

******************************************

Na Jacques Vermeulen

Pamoja na madhara kwa binadamu na kiuchumi, janga la COVID-19 limeleta mtazamo mpya juu ya maendeleo endelevu. Mazingira magumu tunayopitia wanadamu yanatukumbusha kuwa, tukitaka tuishi kwa amani kama viumbe hai, basi tunahitaji kutunza mazingira yetu ya asili.

Kama alivyosema James Quincey, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Coca-Cola hivi karibuni: “COVID-19 imeangazia hitaji la haraka la ushirikiano, kutafuta suluhisho kwa sekta zote juu ya mabadiliko ya tabianchi, taka za plastiki na masuala mengine muhimu ya mazingira na kijamii. Janga hili limetoa mwangaza wa namna dunia ilivyo na muunganiko wa asili hivyo mafunzo tunayoyapata tuyatumie kujijenga na kujiimarisha zaidi ili kufikia mustakabali wa uchumi endelevu na jumuishi. “

Swali dhidi ya anguko kubwa la uchumi unaosababishwa na janga hili, ni jinsi washirika wa kijamii wanaweza kufanya kazi vizuri na kwa umoja katika kuijenga kesho.

Siku ya Uchakataji plastiki duniani inayoadhimishwa Machi 18, inatupa nafasi ya kufikiria upya juu ya jinsi ya kuendeleza ustawi wa Afrika kwa kukuza uchumi wetu pamoja, na kupunguza athari za vifungashio taka kwenye mazingira.

Sehemu kubwa ya jibu ni kujenga uchumi shirikishi wa kijani ambao unaweza kujizungusha na kushirikisha wadau kutoka taasisi za umma na binafsi, jamii na wadau wengine ili kuunda nguvu ya pamoja.

Kwa upande wetu, Coca-Cola Beverages Africa (CCBA), kuchakata plastiki ni kipaumbele chetu cha juu cha kibiashara, pamoja na kipimo muhimu cha utendaji kwa ukuaji wetu na faida.

Kwa maneno mengine, tunapima mafanikio ya biashara yetu sio tu kulingana na ukuaji na faida, lakini pia kwa kufanya biashara kwa njia inayofaa – kufuata maadili yetu na kufanya kazi ambazo hazileti faida tu kwetu bali pia kwa vizazi vijavyo. Faida ni muhimu, lakini sio kwa gharama yoyote. Hatuamini kuwa kuna namna nyingine ya kufaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa mara ya kwanza tokea kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo March 21,2021nya biashara kwa usahihi.

Maono yetu ni kuwekeza katika sayari yetu na ufungashaji wetu ili kusaidia shida ya ufungashaji bidhaa isiwe tatizo tena kwa ulimwengu na mazingira.

Kampuni ya Coca-Cola na wazalishaji washirika wake kwa ujasiri na kujitolea wana lengo la kukusanya na kuzichakata chupa zote za plastiki au za kopo tunazouza mpaka ifikapo mwaka 2030. Tunataka kuunga mkono malengo ya usimamizi wa taka kwa serikali za mitaa kwa kufikia azma ya ukusanyaji na uchakataji wa plastiki kwa asilimia 100% ifikapo mwaka 2030.

Mfumo wa kampuni una lenga kuhakikisha kuwa asilimia 100% ya vifungashio vyetu vinakusanywa kutoka kwa wateja wetu dunia nzima na kuchakatwa upya ifikapo mwaka 2025 na tutumie angalau asilimia 50% ya malighafi iliyochakatwa kwenye vifungashio vyetu ifikapo mwaka 2030. Hii ni sehemu ya mkakati wetu mkubwa wa kukua kibiashara tukiwa kama kampuni ya vinywaji baridi.

Katika masoko yote 14, ambayo CCBA inafanya kazi, tuko njiani kufikia malengo haya kabla ya muda uliopangwa.

Ufumbuzi wa kudumu kwa changamoto kama za ufungashaji wa taka unahitaji ushirikiano katika kuhakikisha tunaleta mabadiliko ya uchumi jumuishi na endelevu katika bara letu.

Kwa upande wao, serikali inaweza kuchangia kwa kuweka mazingira wezeshi ya kisheria na sera kusaidia kuchochea uchakataji endelevu.

Mamlaka pia zina jukumu muhimu katika kuwezesha ushirikiano wa sekta za umma na binafsi, kuweka viwango vya ufungashaji na sera ambazo zinahimiza uchumi wa uchakataji ili kujenga uchumi jumuishi kwa watu.

Tunachohitaji ni kwa jamii, nchi, serikali na wasimamizi kuharakisha mabadiliko kuelekea mitindo ya biashara ya uchakataji. Walakini, ili iweze kutekelezwa kwa mafanikio inahitaji viwango vya juu vya ushirikiano.

Tunaamini kuwa dhana ya Wajibu wa Ziada wa Mzalishaji (EPR) ni njia bora zaidi ya kusaidia uchumi unaozingatia athari za mazingira (duara). Kulipa ada ya EPR na kujitahidi kutumia zaidi plastiki zilizo rejeshwa/chakatwa husaidia sana ingawa ni ghali kuliko plastiki ghafi, maana huwezesha uchumi wa uchakataji (duara).

PETCO ni mfano mzuri – mtindo huu ulianzishwa nchini Afrika Kusini mnamo 2004 kama mpango unaoongozwa na tasnia ya kukusanya na kuchakata chupa za plastiki (PET). Huduma hii ipo Kenya na Ethiopia. Nchini Tanzania, mbali na kuwezesha kuchakata chupa nyingi za Plastiki (PET) kupita zilizouzwa sokoni mnamo mwaka 2020, Coca-Cola Kwanza, kampuni yetu tanzu inayofanya kazi nchini pia imeshirikiana na wazalishaji wengine wa vinywaji baridi ili kusajili Kampuni ya ndani ya PET Recycle (T) Limited (PETCO Tanzania) ambayo itazinduliwa hivi karibuni.

Tunajua kuwa kwa uchumi unaoendelea gharama hizi zinaweza kuwa changamoto kwani zinaweza kuongeza gharama katika kiwango cha mtumiaji. Walakini, muundo huu wa biashara unafaa zaidi katika kutunza thamani ya bidhaa.

Hii ndio sababu tunaunga mkono utumiaji wa plastiki inayochakatika ndani ya mfumo wa Coca-Cola ili tuweze kuunda chupa mpya kutoka kwenye chupa zilizochakatwa.

Afrika endelevu zaidi, yenye umoja zaidi, isiyo na taka, inawezekana ikiwa tutafanya kazi pamoja kwa kushirikiana kwa faida ya pamoja ya bara letu.

* Vermeulen* ni Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Beverages-Afrika