Mratibu wa Mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu Frank Samson akitoa mada kwenye mafunzo ya mwalimu wa darasa la awali wilaya ya Chamwino.Picha na Maktaba
………………………………………………………………………………………………
Na Joyce Kasiki,Dodoma
SHIRIKA linaloangazia Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (CiC ) limefanikiwa kuongeza uwezo kwa walimu wa awali katika wilaya za Kongwa na Chamwino na kumudu mbinu za ujifunzaji na ufundishaji wa Elimu ya awali kutoka asilimia 50 Aprili, 2020 hadi kufikia asilimia 70 Disemba, 2020 katika wilaya za Kongwa na Chamwino mkoani Dodoma.
Akizungumza na mwandishi wa kituo hiki Mratibu wa Mradi wa miaka mitatu wa Watoto Wetu Tunu Yetu unaotekelezwa na CiC katika wilaya hizo Frank Samson,alisema matokeo hayo ni kutokana na tathimini fupi iliyofanywa ndani ya mradi huo baada ya walimu hao kupatiwa mafunzo.
Amesema kabla ya mradi vipo vingi zikiwemo mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa darasa la awali ambavyo walimu walikuwa hawavijui ikiwemo kulifanya darasa kuwa changamshi lakini baada ya mafunzo walimu wameongeza uwezo katika eneo hilo na hivyo kuanza kuleta tija katika darasa hilo.
“Hivi sasa kuna uwepo wa madarasa changamshi yenye zana mbalimbali zinazotokana na mazingira kwa shule 232 za Kongwa na Chamwino na hivyo kuwafikia watoto 22,000 wa Elimu ya awali kufikia Februari 2021” amesema Samson
Aidha amesema pia kumekuwa na ongezeko wa uelewa kuhusu elimu ya Awali kutoka asilmia 28 Aprili, 2020 hadi asilimia 65 Disemba, 2020.
Vile vile amesema,shule zote zilizopo kwenye mradi huo zimetwnga madarasa ya watoto wa awali na kuyawekea zanabalimbali na kona za ujifunzaji na ufundishaji ambazo humwezesha mtoto wa drasa hilo kupenda shule lakini pia kuelewa kwa haraka.
Mratibu huyo pia amesema mafunzo hayo yamesaidia kuongeza ushiriki wa wazazi na jamii kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya Awali ikiwemo ushiriki wao katika kutengeneza zana na utoaji wa lishe kwa watoto hao .
“Hali hiyo imefanya uandikishaji na mahudhurio kwa watoto umeendelea kuwa mzuri kutokana na sababu nyingi zikiwemo walimu mahiri wenye mafunzo, utoaji wa lishe na madarasa changamshi lakini pia utoaji wa lishe ya mara kwa mara kwa watoto wa Awali umeongezeka kutoka shule 15 hadi shule 58 Kati ya 58 zilizopo kwenye mradi kwa awamu ya kwanza” amesema
Kwa mujibu wa Mratibu huyo ,mradi kwa kushirikiana na Serikali umegawa vitabu vya Watoto 42,000 vya kujifunzia wakiwa nyumbani pamoja na vitendea kazi vyake lakini pia kwa kushirikiana na Serikali umefanikiwa kuweka mifumo ya maji ya kunawa mikono Kwa shule 46 zilizopo chamwino na kongwa.