Home Mchanganyiko RAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM...

RAIS SAMIA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUAGA MWILI WA HAYATI MAGUFULI

0

Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli wakiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na mikoa jirani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza Jambo na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemedi Suleiman katika Ghafla ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. leo March 20,2021.

Familia ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli   

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam leo March 20,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)