Home Mchanganyiko RAIS SAMIA AANZA NA WAANDISHI WA HABARI

RAIS SAMIA AANZA NA WAANDISHI WA HABARI

0

p> 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akila kiapo cha uaminifu
 

Na
John Mapepele, Dodoma

Tanzania
imeandika historia ya kuwa na Rais mwanamke wa kwanza kwenye nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi tarehe 19 Machi, 2021 kushika wadhifa huo
kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Mhe, Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021.

 

Kwa
Mujibu wa ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, endapo kiti cha Rais
kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kijiuzulu, kupoteza sifa za
uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana namaradhi ya mwili au  kushindwa
kutekeleza kazi za rais, basi
Makamu wa Rais ataapishwa  na
atakuwa Rais kwa muda  uliobaki katika
kipindi cha miaka mitano.

 

Mara
baada ya kula kiapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na majonzi mazito
amezungumza kwa kifupi na kuanza kwa kutoa ratiba ya mazishi ya mwili wa aliyekuwa
Rais, Mhe. John Pombe ambapo amesema kutakuwa na vituo vinne (Dar es Salaam,
Dodoma, Mwanza na Chato) vitakavyotumika kwa ajili ya kuagia ili wananchi wengi
waweze kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao katika kipindi hiki
kabla  ya mazishi rasmi tarehe 25 Machi
2021.

 

“Leo
si siku nzuri ya kwangu kusema, kutokana na kidonda kikubwa moyoni na mzigo
mzito nilionao. Nimekula kiapo katika mazingira tofauti, nimezoea kula kiapo
katika mazingira tofauti, nimezoea kula kiapo katika hali ya nderemo na furaha
lakini leo nimekula kiapo katika hali ya huzuni na masikitiko” amesisitiza Rais
Samia Suluhu Hassan

 

Kama
ilivyotarajiwa na watanzania wengi
kuhitaji faraja na matumaini kutoka kwa Rais huyu mpya baada ya  wimbi jeusi lililotanda ghafla baada ya
jemedari na shujaa  mwanamapinduzi Dkt
JPM  kuanguka, ndivyo ilivyokuwa baada ya
Rais Samia kusoma hotuba yake fupi iliyosheheni mwanga wa matumaini mapya kwa
Taifa iliyosisitiza  upendo, mshikamano
na umoja kwenye kipindi hiki cha maombolezo.

 

“Katika
kipindi hiki cha maombolezo, ni kipindi cha kuzika tofauti zetu, huu ni wakati
wa kuwa wamoja, huu si wakati wa kutazama yaliyopita, huu si wakati wa
kunyosheana vidole bali huu ni wakati wa kutazama mbele kwa matumaini na kuweka
mbele nguvu kwa pamoja ili kujenga Tanzania ambayo Mheshimiwa Magufuli
aliitamani, na zaidi sana tuungane kumwombea (hayati John Pombe Joseph Magufuli)
alale pema peponi.” Amefafanua

  

Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Samwel Malecela  amesema Taifa linapitia katika kipindi kigumu
jambo la muhimu  ni kuendelea kushikamana  kama watanzania ili kupita kwenye kipindi
hiki kwa umoja na upendo.

 

Mkuu
wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro anaona kuwa pamoja na kuondokewa na
Jemedari Mkuu hayati Dkt. John Pombe Magufuli Mungu ataivusha nchi yetu
itaendelea kuwa imara.

 

“Taifa
hili ni imara,Mungu amelipendelea sana, halikuwahi kuyumba wala kutetereka
katika nyakati zote za changamoto; yalipotokea maasi ya kijeshi mwaka 1964, alipofariki
Mzee Karume mwaka 1972, nyakati mbaya za njaa, nzige na vita ya Uganda miaka ya
1970 na 1980, alipofariki Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine mwaka 1984 na
alipong’atuka madarakani na kufariki Muasisi na Baba wa taifa letu Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere. Tusiogope na tusitetereke, sisi ni taifa imara siku
zote,nyakati zote” anaongeza Mtaturu.

Rais
Samia ameyashukuru makundi ya watu mbalimbali kwa  kuendelea
kushikamana na Serikali yake, makundi hayo  ni pamoja na Chama cha Mapinduzi,viongozi
wakuu wastaafu, vyombo vyote vya ulinzi na usalama na viongozi wa dini.  

Pia
kwa namna ya pekee amewashukuru Wasanii na Waandishi wa Habari kwa kuendelea
kutumia taaluma zao katika kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimmoja wakati
wote. Baadhi ya Wasanii wakongwe wa muziki na Waandishi wameonekana kuguswa
sana na hotuba hii na kutoa ya moyoni:

“OOOh,
No. ungekuwepo wakati tunaangalia hii hotuba ilibidi tukae tuangalie kwenye
luninga, mimi binafsi nilikuwa ninanena kwa lugha nakumbuka nilikuwa
nimezungukwa na vijana nikawamuru watulie kwa sababu  huu ndiyo wakati wa bwana, nikawambia Mungu
alipotaka kuwakomboa Taifa la Israel toka kwenye nchi ya utumwa alimtumia
mwanamke na kwamba aliweka hekima ndani ya mwanamke na wakati huu Mungu ameweka
mwanamke kwa maana kuna jambo ambalo Mungu anataka kutuingiza” amesema
Christina Shusho, mmoja wa waimbaji wakongwe wa nyimbo za Injili hapa nchini.

 

“Mimi
napenda kwenda na neno la kinabii Mheshimiwa Rais Samia ametuheshimisha sana
wasanii wa Tanzania maana kuna makundi mengi lakini sisi wasanii tumependelewa
tumetajwa katika hotuba ya kwanza natambua makundi mengine yataendelea kutajwa”
ameongeza Shusho.

 

Kuhusu
kifo cha Dkt. Magufuli Shusho amesema hayati Rais Magufuli  hakuona haya kumtambulisha Mungu wake katika
kila hatua aliyopita pamoja na nafasi aliyokuwa nayo:

 ” kuna watu ambao
tunampenda Mungu tunamjua Mungu tunapokuwa chini, tukiinuliwa hivi kama  mimi wa bwana Yesu asifiwe unakuta vinapungua
kwa sababu ya position niliyoipata
lakini Mheshimiwa Rais JPM hakumwacha kumsema Mungu wake wakati yeye ndiye
alikuwa kiongozi Mkuu namba moja katika nchi yetu”.

Mwanamuziki
Nguli nchni, Mrisho Mpoto amesema Wasanii na Wanamuziki wataendelea kumkumbuka
Dkt. Magufuli kwa kuwa hakuwabagua, kila msanii alimfanya sawa na mwingine
kiasi cha kumfanya kila msanii ajione anapendwa na Rais JPM.

“Utakumbuka  mtindo wake wa kuwavisha kofia yake alijitahidi sana kwa kadiri alivyoweza kufanya hivyo kwa kila msanii, mimi binafsi aliwahi hata kunitambulisha kuwa ni mwanamuziki  bora kabisa na  yeye ni shabiki
wangu na kwenda mbali zaidi kwa kuimba  baadhi ya nyimbo zangu mbele ya umati wa  watu” amesema Mpoto kwa furaha

Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Dotto Mwaibale amesema falsafa ya Dkt. Magufuli ya kuenzi lugha ya Kiswahili duniani umewafanya hata Viongozi wakuu barani afrika kufikiria kuanza Kiswahili kama lugha rasmi katika nchi hizo

Mwandishi wa Makala haya ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo anapatikana katika: [email protected] gmail.com
au 0784441180