Home Mchanganyiko Majonzi: Dk. Mwaiselage aongoza watumishi Ocean Road kumuaga Dk. Kilongola 

Majonzi: Dk. Mwaiselage aongoza watumishi Ocean Road kumuaga Dk. Kilongola 

0

*************************************

Na Mwandishi Maalum

Watumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dk. Julius Mwaiselage wameuaga mwili wa Dk. Christopher Samwel Kilongola, jana Machi 18, 2021.

Ibada ya kumuaga Dk. Kilongola aliyefariki dunia Machi 16, 2021 imefanyika katika Taasisi hiyo, ambako alilazwa kwa matibabu kabla ya umauti kumfika.

Akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa daktari huyo, Dk. Mwaiselage amesema enzi za uhai wake marehemu alikuwa akifanya kazi katika Taasisi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa bidii, ueledi, na ubunifu sana ambapo wagonjwa wengi walikuwa wanapenda wahudumiwe naye. “Alipenda sana kuwahudumia wagonjwa wote hadi akapata hamasa ya kujiendeleza kusomea masomo zaidi katika saratani”

“Baadae aliacha kazi na kujiunga na Masomo ya Uzamili ya fani ya Onkolojia katika Chuo kikuu cha MUHAS, ambapo sehemu kubwa ya Masomo yake alikuwa akiyapatia akiwa katika Taasisi ya Ocean Road, hakika Taasisi na Taifa imepoteza hazina kubwa” amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga ORCI, Dk. Crispin Kahesa amesema Dk. Kilingola alikuwa mtu anayejituma, na mwenye upendo kwa kila mtu, na ufanisi wa kazi wenye weledi. 

Amebainisha Dr. Christopher anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Mbezi-temboni leo Ijumaa Mchana Machi 19, 2021.