Home Mchanganyiko TAMIDA; TUMEJAWA NA SIMAZI HAYATI RAIS DKT MAGUFULI ALIKUWA JEMEDARI WETU KATIKA...

TAMIDA; TUMEJAWA NA SIMAZI HAYATI RAIS DKT MAGUFULI ALIKUWA JEMEDARI WETU KATIKA BIASHARA YA MADINI.

0
Mwenyekiti wa taifa wa wafayabiashara wa madini Tanzania Sammy Mollel akiongea na waandishi wa habari.
************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mwenyekiti wa taifa wa wafayabiashara wa madini Tanzania Sammy Mollel ameeleza kuwa wamepokea kwa masikitiko makibwa na simanzi taarifa za kifo cha hayati Rais Dkt John Magufuli kwani alikuwa jemedari wao katika kusimamia biashara ya madini. 
Mollel aliyasema hayo wakati akiogea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa hawakuamini walipopata taarifa za awali lakini baada ya makamu wa Rais mama Samia Suluhu kutangaza ndipo wakagundua kuwa ni kweli.
“Kifo cha hayati Rais Dkt Magufuli kimetugusa saa wafanyabiashara wa madini jitihada na maono yake yalipandisha makusanyo ya tozo za madini kutoka millioni 160 kwa mwaka hadi kufikia billioni 2,”Alisema Mollel. 
Alisema wameona juhudi zake binafsi za kujengwa ukuta Mererani ambapo mpaka sasa wameona faida kubwa sana za ukuta huo ikiwemo kulinda usalama wao wanapokuwa katika kazi zao tofauti ma awali, uzalishaji kuongezeka pamoja tozo za serikali kukusaywa kwa kiasi kikubwa. 
“Ameifanikisha sana sekta  ya madini kwa kuelekeza masoko ya madini yajengwe kila mkoa wenye shughuli za uchimbaji madini, tulimweleza kero zetu kuhisiana tozo sumbufu, alizipokea na kutoa maelekezo kwa Bunge kurekebisha ambayo ilikuwa ni tozo ya ongezeko la thamani, VAT na tozo ya zuio na kushuka kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 5,” Alieleza. 
Alifafanua kuwa walimpenda sana lakini Mungu alimpenda zaidi na kama Tamida wanawasihi watanzania kuwa na subira kipindi hiki cha maombolezo na kuyaezi yale yote aliyowaachia kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuigia katika uchumi wa juu. 
“Kwa sababu yake leo Tanzania tuna heshima kubwa sana duniani kwa kuingia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda na sisi tunaahidi  tutamuenzi kwa kuongeza dhamani ya madini na kufika mbali zaidi kama alivyotuazishia,”Alieleza.