*****************************
March 18
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Baadhi ya wananchi mkoani Pwani ,wamesema kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,hayat dkt.John Magufuli kimewaacha midomo wazi ,na kudai watamkumbuka zaidi kwa kuwaachia miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo kupanuliwa kwa barabara kuu ya Morogoro na mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji STIGO.
Aidha wamemtakia mema makamu wa Rais Samia Suluhu safari yake ya kuongoza nchi kuendeleza alipopaacha dkt.Magufuli na kumtakia kwenda na kasi waliyoianza pamoja katika awamu ya tano .
Sophia Daniel,Makelele na Muhammad Patrick walisema kuondokewa na Magufuli wamepigwa butwaa kwani ni kifo cha ghafla.
Makelele alifafanua, hayat Magufuli ameondoka Taifa likiwa bado linahitaji uongozi wake uliojaa uadilifu na kupigania na kutetea wanyonge wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ,madereva boda ,kundi la vijana wanawake na wazee na walemavu.
“Nilishindwa kujivumilia usiku niliposikia taarifa kutoka kwa makamu wa Rais kupitia TBC ,nilistukia naangua kilio,huyu baba kama hujaguswa na msiba wake utakuwa na matatizo” alisema Makelele.
Kwa upande wake mkazi wa Mlandizi,Muhammad alisema mkoa wa Pwani umebaki na kovu ,na wanakumbuka mengi yaliyofanywa kimkoa katika miradi mikubwa ya kimkakati.
Magufuli alitekeleza mengi kimkoa ikiwemo mradi wa reli ya kisasa SGR ni Mradi unakwenda kufungua fursa za kiuchumi kwani umepita ndani ya Mkoa huo kwa asilimia 60.
“Faida nyingine tunayoenda kuipata kwa nguvu zake na uongozi wake ni gati la Nyamisati,meli ya Mafia ,SGR, ,elimu bure,vituo vya Afya ,Maji Kisarawe ,Barabara ya Makurunge – Pangani ,Ukarabari wa Shule kongwe ,Umeme Vijijini serikali imetumia mamilioni ya fedha kuwezesha Vijiji 253 kupata Umeme.
Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini Elina Mgonja ,alimlilia Dkt.Magufuli na kusema wana CCM kijumla na UWT wamepata pigo kubwa .
Alisema kifo ni kazi ya mungu lakini wataendelea kukumbuka mazuri ambayo ni mengi aliyoyafanya dkt Magufuli katika uongozi wake .