Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Mwakiposa Kihenzile(Mb) huku ikiwa imeambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe wakipata maelezo wakati wakikagua ujenzi wa kiwanda cha Hester Bioscience Limited kitakachozalisha chanjo za Mifugo kwa magojwa mahsusi barani Afrika, Chanjo zitakazozalishwa ni Jamii ya Kuku, ng’ombe, kondoo, mbuzi na nguruwe. Kibaha, pwani. Machi 16, 2021
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikikagua na kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha Tanzania Bio – Tech products ltd (TBPL) ambacho huzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneaza ugojwa wa Malaria, kiwanda hiki kimejegwa na Serikali ya Tanzania kwa aslimia 100 kwa kutumia teknologia kutoka nchini Cuba. Kibaha, pwani. Machi 16, 2021
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiangalia na kupokea maelezo ya teknalogia ya kusindika maji ya mhogo na kuengeneza kilevi (alcohol) ambayo ni maligahafi ya kutengeneza vitakasa mikono, ubunifu na teknologia hiyo umetengenezwa na Shirika la utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Dar es salaam. Machi 16, 2021
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikijionea utengenezwaji wa tiba ya COVIDOL inayodhibiti mafua, homa, kifua, aleji, damu kuganda mwilini na kuimalisha kinga ya mwili uliopo chini Shirika la utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Dar es salaam. Machi 16, 2021
Baadhi ya majengo yanayojegwa kwenye Kiwanda cha Hester Bioscience Limited kilichopo eneo la uwekezaji la Shirika la Taifa la (NDC), kiwanda cha Hester Bioscience Africa Kibaha na kitazalisha chanjo za Mifugo kwa magojwa mahsusi barani Afrika, Chanjo zitakazozalishwa ni Jamii ya Kuku, ng’ombe, kondoo, mbuzi na nguruwe na kitazalisha chanjo 37 za wanyama na ujenzi wa kiwanda mpaka kukamilika kitaghalimu Dola za Kimarekani Milioni 18 sawa na bilioni 42 za Kitanzania. Kibaha, pwani. Machi 16, 2021
Picha zote na Eliud Rwechungura
****************************************
Na Eliud Rwechungura
Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. David Kihenjile (Mb) na Makamu Mwenyekiti Mhe. Eric Shigongo imeambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) katika mwendelezo wa ziara za kamati hiyo katika mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es salaam kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni moja ya kazi za kamati za Bunge
Katika Mkoa wa pwani, Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imetembelea maeneo mawili ambayo ni ujenzi wa Kiwanda cha Hester Bioscience Limited kilichopo eneo la uwekezaji la Shirika la Taifa la (NDC), kiwanda cha Hester Bioscience Africa Kibaha na kitazalisha chanjo za Mifugo kwa magojwa mahsusi barani Afrika, Chanjo zitakazozalishwa ni Jamii ya Kuku, ng’ombe, kondoo, mbuzi na nguruwe na kitazalisha chanjo 37 za wanyama na ujenzi wa kiwanda mpaka kukamilika kitaghalimu Dola za Kimarekani Milioni 18 sawa na bilioni 42 za Kitanzania
Eneo la pili kamati imetembelea na kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha Tanzania Bio – Tech products ltd (TBPL) ambacho huzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneaza ugojwa wa Malaria ambapo kiwanda kinategemea kuingia kwenye awamu ya pili ya uzalishaji wa viatifu (biopestide), kiwanda hiki kimejegwa na Serikali ya Tanzania kwa aslimia 100 kwa kutumia teknologia kutoka nchini Cuba
Pia katika Mkoa wa Dar es salaam, Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imetembelea makao makuu wa Shirika la utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) na kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea katika shirika hilo ambapo imejonea teknologia na mitambo mbalimbali iliyoundwa na kutengeneza na taasisi hiyo.
Awali kamati imejionea teknalogia ya kusindika maji ya mhogo na kuengeneza kilevi (alcohol) ambayo ni maligahafi ya kutengeneza vitakasa mikono Pia utengenezwaji wa tiba ya COVIDOL inayodhibiti mafua, homa, kifua, aleji, damu kuganda mwilini na kuimalisha kinga ya mwili.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Eric Shigongo kwa niaba ya kamati hiyo ameipongeza serikali kwa kukaribisha wawekezaji kwa kujenga kiwanda kikubwa Afrika cha chanjo za mifugo kitakachotoa ajira kwa watanzania na wafugaji watakuwa na uhakika wa chanjo zitakazozalishwa ndani ya nchi huku akiipongeza serikali kwa kwa kujenga kiwanda cha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu na kusisitiza kuwa “katika nchi ni vyema tukawekeza sana katika tiba ya kufanya magojwa yasitokee” pia akisisitiza kiwanda kulipa mishaara ya wafanyakazi kwa wakati na akimaliza kwa kupongeza Shirika la utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kwa kufanya tafiti ambazo zimefanywa na watanzania na zimesaidia kubuni na kuzalisha vitu mbalimbali, mafano dawa ya asili ya Covidol.
Nae, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe (Mb) amepongeza kampuni ya Hester Biosciences Af rica kwa kuwekeza kwenye kiwanda kikubwa barani Afrika cha kuzalisha Chanjo za mifugo, pia amesema serikali itaendelea kuweka nguvu katika kiwanda cha Tanzania Bio – Tech products ltd (TBPL) kinachozalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneaza ugojwa wa Malaria ili kupambana na kutokomeza kabisa ugojwa wa malaria huku akiipongeza taasisi ya TIRDO kwa kuendelea kufanya utafiti pia ubunifu na uzalishaji wa tiba ya asili ya Covidol ambayo imesaidia kupamabana na Corona sambamba na matatizo ya kupumua huku akihitimisha kwa kuihakikisha kamati kuwa Seikali itayafanyia kazi maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na kamati hiyo.