Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kulia) leo wakati alipozindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo ukanda wa Kusini (SAGCOT) Dkt. Geofrey Kirenga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kizimba Business Model leo unaofanywa na SUGECO mjini Morogoro ambapo amesema taasisi yake inafanya kazi ya kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kwenye kilimo hususan vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw. Revocatus Kimario amesema mfumo wa Kizimba Business Model unalenga kuwavutia vijana washiriki kwenye kilimo kwa kubadili fikra na mitazamo kuona kilimo ni ajira na biashara kama ilivyo kwa watumishi wengine.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akitazama bidhaa inayotengezwa na mjasiliamali Fatma Mbaga (kushoto) chini ya usimamizi wa SUGECO ikiwa ni mkakati wa kukuza biashara ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji SUGECO Revocatus Kimario.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine Prof. Raphael Chibunda akizungumza kwenye uzinduzi wa Kizimba Business Model leo Morogoro amesema mfumo huo chini ya SUGECO unalenga kusukuma na kubadili kilimo kuwa cha kibiashara na kuvutia vijana wengi zaidi kushiriki.
Waziri wa Kilimo Prof. adolf Mkenda akizindua mfumo wa kilimo ujulikanao “Kizimba Business Model ” unalenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO leo mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (katikati) akitazama trekta linalotumika kufundishia vijana kilimo biashara leo alipozindua mfumo wa Kizimba Business Model makao makuu ya Taasisi ya SUGECO Morogoro yenye lengo kuuunganisha vijana kufanya kilimo biashara.