Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Sizya Tumbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini kwa kutumia tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali wa ushirika, kongamano linafanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Dkt Benson Ndiege akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini kwa kutumia tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali wa ushirika, kongamano linafanyika kwa siku tatu jijini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha ushirika Moshi Prof. John Safari ambao pia ni washiriki katika kuandaa kongamano hilo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini kwa kutumia tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali wa ushirika, kongamano linafanyika kwa siku tatu jijini.
Meneja ushirika mradi wa Pamoja wa Tumbaku Morogoro (TCJE) Bw. Bakari Hussein akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini kwa kutumia tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali wa ushirika, kongamano linafanyika kwa siku tatu jijini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Sizya Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini kwa kutumia tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali wa ushirika, kongamano linafanyika kwa siku tatu jijini.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Jijini Dodoma, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
***************************************
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe ameagiza tafiti zinazofanywa kwenye sekta ya ushirika kuwasilishwa kwa lugha adhimu ya Kiswahili ili iweze kufahamika na wadau na watumiaji wa tafiti hizo ili kuinua sekta hiyo ili iweze kuleta tija.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma kwenye taarifa ya Naibu Waziri Bashe iliyosomwa kwa niaba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Sizya Tumbo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kwanza la tafiti za Ushirika wanaokutana Dodoma kuona namna ya kuboresha ushirika hapa nchini.
Amesema tafiti nyingi zinazohusiana na sekta ya ushirika zimekuwa zikifanywa na taasisi, Vyuo vya elimu na watu binafsi na zimekuwa zikitoa mapendekezo mbalimbali ya namna ya kuboresha ushirika lakini tafiti hizo zimekuwa zikiishia kuchapishwa na kuhifadhiwa kwa kuwa si rafiki kwa watumiaji.
“Tafiti zinazohusu masuala ya sekta ya ushirika ziwasilishwe kwa lugha ya Kiswahili ili iwe rahisi kutumika na vyama vya ushirika, tafiti nyingi zimekuwa zikiwasilishwa kwa lugha ya kiingereza ambayo si rafiki kwa wanachama wengi wa ushirika” amesema.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha vyama vya ushirika vinanufaika na matokeo ya tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali ili kuinua utendaji na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya ushirika hapa nchini ili kupata tija iliyotarajiwa.
Amewataka washiriki wa kongamano hilo waweke mikakati ya kutatua changamoto kupitia tafiti zinazofanywa ili kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa vyama vya ushirika na hivyo kuchochea ubunifu katika maeneo ya uzalishaji na uongezwaji thamani wa mazao.
Aidha ameagiza tafiti zinazofanywa na wadau wa maendeleo ya ushirika ziwasilishwe katika ofisi ya tume ya maendeleo ya ushirika na ofisi ya Mrajis wa vyama vya ushirika ihakikishe mapendekezo yanafanyiwa kazi na kuwasilishwa kwenye vyama vya ushirika.
Tume ya maendeleo ya ushirika na wadau wa maendeleo ya ushirika iongeze rasilimali zinazowezesha tafiti za ushirika kufanyika kwa ufanisi zaidi, na makongamano kama hayo yafanyike kila mwaka ili kujadiliana matokeo ya utafiti zilizofanyika ili kupima utekelezaji yale yaliyoadhimiwa.
Awali Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Dkt Benson Ndiege amesema kongamano hilo ni la siku tatu linaloshirikisha washiriki zaidi ya mia nne (400) pia maada mbalimbali zitawasilishwa zinazohusu utafiti zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina ya namna ya kuboresha ushirika.
Amesema lengo la kongamano hilo kuona namna ya kufufua na kuboresha ushirika na kuimarisha ushirika hapa nchini na baada ya kongamano hilo kutakuwa na mabadiliko makubwa sana katika utendaji na kuongeza uelewa zaidi.
Ameongeza kuwa “siku hii ya leo ni muhimu sana kwa tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania, chuo kikuu cha ushirika Moshi, wanaushirika Pamoja na wadau wote wa ushirika ni siku ambayo tunaianza safari yetu ya kutumia matokeo ya utafiti zilizofanyika awali kuondoa changamoto za ushirika” amesema.
Akitoa neno la shukrani Meneja ushirika wa mradi wa pamoja tumbaku Morogoro bw. Bakari Hussein amesema kongamano hilo limekuwa msaada mkubwa kwao na litaleta majibu ya maswali mengi katika ushirika, na kupongeza agizo la tafiti kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili kwani awali ilikuwa kikwazo tafiti zilikuwa katika lugha ambayo si rafiki kwa watumiaji wa tafiti hizo.