Home Michezo TAIFA STARS YALALA BAO 2-1 DHIDI YA HARAMBEE STARS

TAIFA STARS YALALA BAO 2-1 DHIDI YA HARAMBEE STARS

0

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO

Leo timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ilishuka dimbana kumenyana na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars kwenye mechi ya kirafiki na kushuhudia taifa stars ikilala kwa mabao 2-1 kwenye mchezo huo.

Harambee Stars ilianza kuapta bao dakika ya 21 kupitia kwa nyota wao Kapaito na kuongoza mpaka dakika ya 39 Taifa Stars kusawazisha kupitia kwa Ayoub Lyanga na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili timu ya taifa ya Kenya iliingia ikiwa inahitaji bao la lingine na kuweza kufanikiwa kupitia kwa nyota wao Abdallah dakika ya 58.