Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na wajumbe wa kikao maalumu cha kamati ya Ushauri cha Mkoa ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya kuweza kupitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa kuanzia 2021 /2022 kilichohudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa dini na wadau wa taasisi za umma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere akizungumza jambo katika kikao hicho amabcho kiliandaliwa mahusus kwa ajili ya kuweza kujadili na kupitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya Mkoa huo kwa kipindi cha mwak 2021 hadi 2022.
Mchumi wa Mkoa wa Pwani Gerald Mbosoli wakati akisoma taarifa ya mapendekezo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha kwa kipindi cha 2020 /2022.
Mmoja wa mjumbe wa kikao hicho maalumu cha mapendekezo ya bajeti ya Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mafia, akichangia mada juu ya mwenendo mzima wa vipaumbele amabvyo vimeelezwa katika bajeti hiyo,
********************************************
NA VICTOR MASANGU ,PWANI
KIKAO maalumu cha kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Pwani kimeazimia kwa pamoja kupitisha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mia 298 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa kuanzia 2021 /2022 ambacho kimeombwa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake mbali mbali ikiwemo mishahara ya watumishi pamoja na ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Mchumi wa Mkoa wa Pwani Gerald Mbosoli wakati akisoma taarifa ya mapendekezo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha kwa kipindi cha 2020 /2022 ambapo kilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,viongozi wa dini ambao kwa pamoja waliweza kuiunga nga mkono bajeti hiyo kwa asilimi 100 ambayo itakwenda kuleta chachu ya maendeleo.
Alibainishwa kwamba kiasi hicho kilichoombwa kinaongezeka kwa kiasi cha asilimia 9.38 ikilinganishwa na bajeti inayoendelea kutekelezwa na kwamba maeneo amabyo yameongezeka ni katika matumizi mengineyo katika sekretarieti ya Mkoa ikiwemo upande wa mishahara ya halmashauri pamoja na mapato ya ndani.
Aidha Mchumi huyo wa Mkoa alisema kwambaa licha ya bajeti hiyo kupitishwa kwa kishindo na wajumbe lakini kumekuwepo na baadhi ya chanangamoto katika suala zima la mianya ya utoroshaji wa mapato kutokana na uwepo wa bandari bubu pamoja na njia ambazo sizizo rasmi.
Pia alisema kwamba sababu ambazo zinapelekea kutofikia malengo katika ukusanyaji kwa baadhi ya halmashauri ni kushindwa kukusanya ushuru wa madini ya ujnenzi pamoja na baaadhi ya wananchi wengine kutokuwa tayari kwa ajili ya kulipia kodi na ushuru wa hiari.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kwamba mpango wa bajeti hiyo pindi itakapotistishwa Waziri mwenye dhamana itakwenda kuleta mabadiliko chanya zaidi kwa wananchi katika suala zima la kimaendeleo na kwamba ana matumaini makubwa ya mapendekezo hayo ya bajeti yataweza kuwa ni mkombozi katika kuhudumia sekta mbali mbali.
Pia Ndikilo ameziomba halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba wanaweka mipango madhubiti ya kuweza kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato kulikwa kutegemea chanzo kimoja katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.
“Kitu kikubwa ninacho waomnba wakurugenzi wa halmashauri zote tisa zilizopo Mkoa wa Pwani ni lazima sasa tuweze kupambana zaidi katika ukusanyaji wa mapato maana kuna baadhi ya halmashauri hapa bado hazijatimiza malengo amabayo yamewekwa na serikali naona nyingi bado zipo chini ya asilimia 50 na chache tu ndio zimeweza kuvuka juu ya asilimia 50.”alifafanua Ndikilo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere alisema kwamba katika kipindi cha mwaka wa 2021/2022 mkoa wa Pwani utakuwa ni vipaumbele vipatavyo tisa ikiwemo kuhakikisha kwamba inasimamia hali ya ulinzi na Usalama, kusimamia utekelezaji wa mkakati wa Taifa dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa.
Kadhalika aliipongeza serikali ya ya awamu ya tano kwa kuweza kutatua baadhi ya chagamoto ikiwemo kutekeleza ujenzi wa bandari ya Nyamisati, Kivuko cha kisasa cha Mv- Kilindoni, kutoa magari 11 kwa ajili ya wakuu wa Wilaya pamoja na makatibu Tawala wa Wilaya ambayo yameweza kuwa mkombozi mkubwa katika utekelezaji wa makukumu ya ya ya kuwatumikia wananchi.
Pia alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kusimamia utekelezaji wa shughuli za masuala ya mtambuka VVU, ukimwi , magonjwa yasiyo ya kuambukiza, lishe pamoja na mabadiliko mbali mbali ya tabia ya nchi, ikiwemo pamoja na kuimarsiha usimamizai na ufutatiliaji wa ukusanyaji wa mapato, pamoja na kuweza kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani katika halmashauri husika.
Kadhalika alifafanua kwamba vipaumbele vingine vitakuwa ni uandaaji wa mazingira ya uwezehaji kwa ajili ya uwekezaji na ujnezi wa viwanda mbali mbali, pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya elimu pamoja na afya, pamoja na kutilia mkazo zaidi katika sekta ya kilimo mifugo pamoja na masuala ya uvuvi.
Katika hatua nyingine jambo linguine ni kuhakikisha wanasimamia stahiki za watumishi ikiwemo pamoja na ulipaji wa madeni mbali mbali lengo ikiwa ni kuwapa molali zaidi ya watumishi waweze kufanya kazi kwa weledi mbao unatakiwa kwa kuzingatia msingi ya kazi iliyowekwa.
Nao baadhi ya wajumbe waliohudhulia katika kikao hicho walitoa pongezi kwa uongozi mzima wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuweka vipaumbele mbali mbali ambavyo vitaweza kuwasaidia wananchi wanyonge na kwamba mapendekezo hayo ya mpango wa bajeti yatasaidia kutatua changamoto mbali mbali katika suala la huduma za kijamii sambamba na kuwapatia watumishi stahiki zao.