***********************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa mkoa wa Tanga kufanya jitihada na kuongeza nguvu katika kumalizia chuo cha ufundi stadi VETA ili kuchukua vijana wa Tanga watakaoweza kujiunga na Chuo hicho kupata ujuzi mbalimbali
Ameyasema hayo leo Mhe.Samia baada ya kuweka jiwe la msingi katika chuo cha Ufundi stadi VETA kilichopo eneo la mtonga Wilayani Korogwe.
Awali akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt.Pancras Bujulu amesema kuwa mradi huo umeanza utekelezaji wake machi 23 ,2020 utagharimu sh 1,6 bilion. ambapo mradi huo unatekelezwa na VETA kwa kutumia nguvukazi ya ndani (force account) Kupitia chuo cha VETA kihondo kilichopo Mkoani Morogoro
kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 60 ya utekelezaji ambapo utakapokamilika unatarajiwa kudahili wanafunzi 240 kwa kozi za muda mrefu na wanafunzi 620 wa kozi za muda mfupi kwa mwaka
Nao baadhi ya wananchi wamesema kuwa ni furaha kwao kupata chuo hicho katika wilaya ya korogwe kwani kitawapa fursa vijana kujifunza ufundi stadi utakoawasaidia katika kupata ujuzi mbalimbali na kujikwamua kiuchumi
Mkoa wa Tanga unaingia katika historia kwa kuwa na vyuo vingi vya Ufundi stadi ambapo vimekua vikitoa ajira na kuwasidia vijana wengi katika urasimishaji wa ujuzi wa fani mbalimbali.