Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba Akifanya mazoezi katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa jana,na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, ili kuwahamasisha watumishi na wakazi wa Nyasa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa mbalimbali. Na wengi ni Watumishi wa Wilaya ya Nyasa wakifanya mazoezi Picha na Ofisi Ya DED Nyasa.
****************************
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa jana, wamefanya mazoezi ya viungo, katika Viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma , yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilmba.
Lengo la Kufanya mazoezi ya Viungo kwa Watumishi hao, ni kujenga miili ya Wafanyakazi hao wasishambuliwe na magonjwa ya kifua na kuongeza ari ya Utendaji kazi na kufahamiana.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mazoezi hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Isabela chilumba, amewashukuru na kuwapongeza watumishi wa Halmashauri na Taasisi zote za Serikali waliohudhuria mazoezi, na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kila mara ikiwa ni agizo la mh Samia Suluhu Hasan , Makamu wa Rais wa Tanzania, kama alivyoagiza jumamosi ya pili ya kila mwezi ni siku ya Mazoezi ya Viungo.
Ametoa wito kwa wananchi na watumishi wa Umma kufanya mazoezi binafsi , kila siku ili kujenga miili yao na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kifua, kufahamiana na kujenga ari ya kushirikiana kwa wafanyakazi.
“Leo ni siku ya Mazoezi kwa wakazi wa Wilaya ya Nyasa tunaitumia siku hii kufanya mazoezi ili kuweza kujenga miili yetu, isishambuliwe na magonjwa, lakini pia michezo inasaidia kuleta upendo, na kujenga mshikamano pamoja na kufahamiana, hivyo kama wana Nyasa tunatekeleza, Pia Agizo la Mh,Samia Suluhu Hasan Makamu wa Rais wa Tanzani kwa kuwa ametutaka kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya mwezi na Nyasa Tunatekeleza.
Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi wote, kujitokeza kwa wingi katika mazoezi ambayo yanafanyika kila jumamosi.
Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wamesema wanafurahia sana mazoezi kwa kuwa yanawafanya wawe vizuri kiafya na kuwafanya waongeze ari ya Utendaji kazi.