………………………………………………………………………………………..
Na.Joctan Agustino,Njombe
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Njombe kuanzisha vitaru vya parachichi kupitia fedha za asilimia 10 na Kisha kutoa Miche bure kwa wananchi wanaohitaji kufanya kilimo hicho ili kuinua kilimo Hicho ambacho kinakuwa kwa kasi na kuingiza fedha nyingi za kigeni serikali
Mbali na uanzishwaji wa vitaru vya Miche Waziri mkuu pia amempa agizo katibu mkuu wa wizara ya kilimo kutenga ardhi ya kujenga kiwanda Cha parachichi ili kuongeza thamani ya malighafi hiyo ambayo nahitaji yake katika soko la ndani na nje yanakuwa kila uchwao.
Akizungumza Mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la mkulima wa mfano wa parachichi ambaye pia ni mkulima Bora Kanda ya nyanda za juu kusini 2019 Steven Mlimbila ,waziri Majaliwa amesema serikali imedhamiria kuboresha kilimo Hicho ambacho kipo katika mazao ya bustan.
Awali mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe Neema Sanga wanasema kwa mwaka Jana mkoa ulizalishe tani elfu 7100 hivyo serikali inakila sababu yabkutatua changamoto zinawakabili wakulima ili wapate tija zaidi.
Ujio wa waziri mkuu kwa mkulima huyu anaefahamika kwa jina la Steven Mlimbila Maarufu Nemes unaibua hisia tofauti kwake na kudai kwamba anakwenda kulima zaidi ili afikie lengo la kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 200 hatua ambayo itaipunguzia kazi serikali ya kuajiri.