
Afisa mikopo wa CRDB kanda ya Kaskazini Emmanuel Kafui akizungumza wakati wa tuzo za wanawake zilizofanyika Mkoani Arusha.
……………………………………………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO ARUSHA
Wanawake wametakiwa kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo kwenye benki ya CRDB hasa katika akauti ya Malkia ili wazidi kujikwamua kiuchumi.
Rai hiyo ilitolewa na Afisa mikopo wa kanda ya Kaskazini wa benki hiyo Emmanuel Kafui wakati akizungumza kwenye hafla ya mwanamke tuzo iliyofanyika jiji Arusha ambapo alisema kuwa malkia akaunti ni akaunti maalum kwaajili ya kuwawezesha wanawake kujiwekea akiba na kupata mikopo ya Malkia.
Kafui alisema kuwa huduma hiyo inapatikana katika matawi yote 16 ya CRDB mkoa wa Arusha lakini pia katika kanda nzima na nchi kwa ujumla ambapo mikopo ya Malkia inaanzia laki tani hadi billioni 3.
“CRDB imekuwa ikiwahudumia wateja wake kwa kuangalia mahitaji yao halisi ndio maana tulianzisha akaunti ili kumsaidia mwanamke ambaye tunajua ndio kiungo kikubwa cha kuhakikisha familia na inakuwa bora kwa kujishughulisha na masuala mbalimbali ya kiuchumi,” Alisema Kafui.
Aidha kuhusiana na tuzo za mwanamke alieleza kuwa CRDB inaungana na wanawake katika kuwapongeza wanawake wapambanaji kwa kiwatambua juhudi zao.
Sambamba na hayo pia aliwapongeza wanawake kwa kuwa wateja wazuri wa CRDB na kuwakumbusha kuwa benki hiyo ni benki ya kitanzania na mdau muhimu katika wa maendeleo ya wanawake katika jamii.