Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imepanga kufanya zoezi la upandaji mawe (beacons) na uchakataji wa namba za viwanja sambamba na uandaaji wa hati miliki kwa ajili ya umilikishaji kwa wamiliki wa viwanja hivyo katika Kata ya Dabalo. Aidha, urasimishaji ardhi katika Mji Mdogo wa Dabalo unahusisha mitaa mitatu (3) ya Nayu, Igamba na Dabalo ambapo zoezi hili linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007.
Tangu kuanza kwa zoezi hili Novemba 2020 vipande 3191 vya ardhi vimetambuliwa na michoro kumi (10) ya Mipango Miji yenye jumla ya viwanja 1152, imeandaliwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika. Hii imetoa nafasi ya kuanza kwa hatua ya umilikishwaji ambayo inahusisha upandaji wa mawe na uandaaji wa hati miliki kwa viwanja vinavyopimwa. Zoezi linatarajia kuanza Jumatatu tarehe 15 Machi 2021 katika eneo la Mji Mdogo wa Dabalo.
Mbali na kuwepo kwa viwanja vya makazi katika eneo la Mji Mdogo wa Dabalo lenye mitaa ya Nayu, Igamba na Dabalo, pia kuna mashamba ambapo MKURABITA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wanaendelea na zoezi la urasimishaji wa mashamba ya wakulima wadogo wa miwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999. Zoezi hili linatekelezwa katika Kijiji cha Manyemba chenye jumla ya vitongoji saba (7) ambavyo ni Muungano, Azimio, Mtakuja, Nyerere, Ikulu, Mapinduzi na Mbandee. Aidha, jumla mashamba 107 yamepimwa na uandaaji wa hati za haki miliki za kimila unaendelea sambamba na maandalizi
Empowering the Disadvantaged Towards Expanded Market Economy
ya zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila kwa wenye mashamba na mafunzo ya kuwajengea uwezo wa jinsi ya kuunganishwa na kuduma za ukuzaji wa mitaji na uzalishaji wenye tija.
Hadi kufikia Februari 2021 MKURABITA kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa imefanikiwa kujenga uwezo kwa ajili ya urasimishaji endelevu wa ardhi vijijini katika Halmashauri za Wilaya 57 ambapo jumla ya mashamba 140558 yamepimwa na jumla ya hati za haki Miliki ya Kimila 101,415 ziimeandaliwa katika vijiji 225.
Aidha, urasimishaji ardhi mijini umetekelezwa katika Halmashauri za tisa (9) za Miji, Manispaa na Majiji. Jumla ya viwanja 19,591 vimepimwa na hati miliki 1,452 zimeandaliwa.