***********************************
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshiriki kwenye Mkutano wa Kamati Tendaji (Exucutive Committee) ya Jukwaa la Jumuiya ya Tume za Uchaguzi kutoka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF SADC) wenye lengo la kuimarisha usimamizi wa uchaguzi na kukuza demokrasia nchi.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Rufaa Mstaafu Semistocles Kaijage akichangia hoja za kuimarisha utendaji kazi wa jukwaa hilo.
Katika mkutano huo Mwenyekiti ameungana na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Rufaa Mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk, Mjumbe wa Tume Jaji Mstaafu Mary Longway walioshiriki wakiwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi akiwa jijini Dodoma.
Ajenda kubwa ya mkutao huo ilikuwa ni kupitia Taarifa ya Utendaji Kazi wa Sekretarieti ya Uendeshaji ya jukwaa hilo na kupokea muongozo wa masuala yaliyokubaliwa katika Mkutano Mkuu wa ECF SADC.
Baadhi ya nchi zilizoshiriki katika mkutano huo ni Angola, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Botswana na Shelisheli.
ECF SADC imeundwa na Tume 16 za Uchaguzi kutoka nchi za SADC na Kamati Tendaji yenye wajumbe 6 ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania.
Lengo la jukwaa hilo kubadilishana uzoefu na kuzijengea uwezo Tume wanachama kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa uchaguzi katika nchi wanachama wa SADC na kukuza demokrasia katika ukanda huo.