Kamanada wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa akionyesha baadhi ya vifaa mbali mbali zilivyoikamatwa na jeshi hilo viukiwemo ambayo viliibiwa katika msiba ambao ulitokea katika maeneo ya mlandzi Wilayani Kibaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa akiwaonyesha waandishi wa habari hawapp pichani magunia 12 ya bangi ambayo yalikamatwa katika msako mkali uliofanyika kwa kipindi cha wiki moja mfululizo pamoja na vitu vingine mbali mbali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
…………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU,PWANI
JESHI la polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 23 ambao wamejihusisha katika makosa mbali mbali likiwemo la kufanya uharifu wa wizi wa kuiba vitu mbali mbali katika msiba mmoja ulitokea mlandizi Wilayani Kibaha pamoja na wengine kukutwa na madawa ya kulevy aina ya bangi , wizi wa laini 74 za simu ambazo zilikuwa zikitumika katika kufanyia utapeli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishiwa habari Ofisini kwake amebainisha kwamba matukio hayo yametokea kwa nyakati tofauti na kwamba wezi hao walikwenda katika msiba huo na kukuta watu wamelala ndipo walivunja mlango na kisha kuibgia ndani na kuwapulizia watu dawa.
Wankyo alisema tukio hilo la wizi uliofanyika msibani baada ya mazishi watu wakiwa wamelala ndani wezi walivunja mlango wa nyumba wafiwa wakiwa wamepuliziwa dawa ndipo wezi wakaiba vitu mbali ikiwemo Televisheni tatu, Mbili aina ya Startimes inch 32 na moja aina ya UK inch 21,Simu za mkononi tano. (Tecno 3, Itel 01, Bontel 1)
Alivitaja vitu vingine vilivyoibiwa msibani kuwa ni pamoja na Radio mbili aina ya Sonny Spika nne, Deki mbili. Moja aina ya LS na nyingine aina ya HITACH King’amuzi kimoja aina ya Startimes.
Kamanda Wankyo amesema Jeshi hilo limefanya operesheni kwa kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 01/03/2021 hadi tarehe 10/03/2021 katika Wilaya zote tano za Polisi ambapo Watuhumiwa wengi Kati ya hao 23 walikamatwa huko mlandizi wilayani kibaha.
“Madhumuni ya misako hiyo ilikuwa ni kudhibiti na kuzuia matukio ya makosa ya wizi, Uvunjaji na matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Wankyo.
Katika operesheni hii tumefanikiwa kukamata Watuhumiwa hao walikamatwa na vitu vingine mbalimbali kama Bhangi kilo 296, Miche ya bhangi iliyokutwa imelimwa nyumbani kwa mtuhumiwa katikati ya shamba la mahindi àmbapo mtuhumiwa alikuwa akitunza kwa kupalilia bhangi hizo sawa zao lake la mahindi na pia alikuwa na Mirungi bunda 35 huko wilayani Bagamoyo.
“Laini 74. Kati ya hizo laini 56 ni mpya na laini 18 zinazotumika kufanya utapeli zikiwa zimesajiliwa kwa jina moja la Mosses Cosmas” alisema Wankyo.
Aidha Scanner moja aina ya Mantra kwa ajili ya kuchukua alama za vidole (Finger print) Mashine ya kusajilia laini Solar power, Makoti 12 ya Kampuni ya ulinzi ya SGA, Pikipiki moja aina ya SAN LG nyekundu yenye namba za usajili T.659 CCA Ikiwa ni pamoja na Pombe ya gongo lita 49
Hata hivyo kamanda Wankyo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawahakikishia wananchi kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote na operesheni hizi ni endelevu.
Alisema Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
“Wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria na kuufanya Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa shwari” alisema Wankyo.