Picha ya pamoja ya wadau wa maji Mkoani wa Arusha wakiwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta katika kikao kazi kilichofanyika Mkoani humo. Wadau waaji wakifuatilia jambo katika kikao kazi cha wadau wa maji Mkoani Arusha.
*********************************
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta ametoa rai kwa wadau wa maji mkoa wa Arusha kuongeza kasi katika kiwango cha ukuaji wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa mwaka kwa wananchi waishio vijijini kutoka asilimia 2.1 na kufikia asilimia 3.2.
Kimanta alitoa rai hiyo wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa sekta ya maji vijijini mkoani Arusha uliondaliwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) ambapo alisema kiwa malengo ya serikali ni katika sekta ya maji vijini ni kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio vijijini Hadi kufikia wastani was asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 huku malengo endelevu ya kimataifa yakiwahitaji kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.
Alisema kuwa kwa misingi hiyo wwnahitajika kuongeza Kasi zaidi ili kuweza kufikia malengo hayo na ni matarajio yake kikao hicho kitajenga mikakati ya nguvu za pamoja katika kuwa na Mipango na bajeti jumuishi itayoakisi hitaji halisi la kufikia malengo ya serikali kabla au katika muda uliopangwa.
“Ni dhahiri kila mmoja wetu katika kikao hiki ana ana nafasi yake katika kuwezesha azma ya serikali yetu hivyo ni vyema mipango yenu ikawa wazi kwa kila mmoja ili kuoanisha nguvu za pamoja na kupata matokeo makubwa na ya haraka ili kuendana na Kasi tarajiwa kama nilivyosema apo awali,” Alisema Kimanta.
Alieleza kuwa wasipooanisha mipango yao vizuri upo uwezekano mkubwa wa kufanya kazi ile ile kwa kujirudia bila kujua au kushindwa kuzitumia rasilimali hizo kwa sehemu kubwa zaidi katika maeneo ya vijijini.
Aidha alisema kuwa takwimu za upatikanaji wa maji imeongezeka kutoka asilimia 58.7 kwa mwaka 2015 na kufikia wastani was asilimia 69.2 kwa mwaka 2020 huku vijiji vyenye huduma rasmi ya maji vikiongezeka kutoka vijiji 236 mwaka 2015 Hadi kufikia vijiji 304 304 Kati ya vijiji 390 vilivyopo mkoa was Arusha.
“ Hii inamaanisha kuwa Kuna vijiji 86 ambavyo havina huduma rasmi za maji katika mkoa wetu sawa na asilimia 22.1 hivyo ni vyema kujitadhimini tulipofiki na tulipotoka ili kujenga mikakati yenye kuendana na kasi inayotakiwa hivi sasa ili kuziba pengo lililopo,” Alieleza.
kwa upande wake meneja wa RUWASA mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph Makaidi alisema kuwa katika bajeti ya 2021/2022 ambayo wameomba zaidi ya billioni 17 italenga miradi 15 inayoendelea, miradi mipya 8, ukarabati wa miradi 17 iliyokuwepo, kuendeleza vyanzo 32 kwaajili ya mwaka ujao pamoja na usanifu wa miradi 35.
Alisema kwa katika kikao hicho wataweza kujadili malengo na majukumu yao, kujenga uelewa wa pamoja wa changamoto zilizopo vijijin, kujenga mikakati na kubadilishana uzoefu ili kuweza kupata matokeo mazuri.