Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge,akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge,akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Maduka Kessy,akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai,akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk.Godfrey akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Dodoma wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Mbuge wa Mvumi (CCM) mkoani Dodoma Mhe.Livingstone Lusinde akiwa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mhe.Kunti Majala,wakifatilia kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma
Mhandisi Ofisi ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Fredrick Mageni ,akiwasilisha Mada kuhusu Uanzishwaji wa Majukumu na Muundo wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk.Godfrey Mbabaye akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za RUWASA na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21 kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya RM-Dodoma Bi.Prisalla Mkilanya,akiwasilisha Mada kuhusu Uundaji na Usajiri wa Jumuiya za Usimamizi wa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO’S) kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa pia ni Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai,akichangia jambo wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kongwa Bw.Musa Abdi,akichagia Maga wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Mbuge wa Mvumi (CCM) mkoani Dodoma Mhe.Livingstone Lusinde akieleza jambo wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini Mhe.Ally Makoa akichagia Mada wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Wialya ya Bahi Stewart Masima ,akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Sekta ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Dodoma kilichofanyika leo March 9,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ameutaka Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Mkoa wa Dodoma katika bajeti yake kwa mwaka 2021/2022 kukutana na kila Halmashauri ili kujua mahitaji yao ili katika bajeti hiyo ilenge mahitaji mahususi ili kupunguza uhaba wa maji kwa wananchi.
Dkt Mahenge ametoa wito huo Leo March 9,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha wadau wa sekta ya maji na usafi wa mazingira vijijini Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na RUWASA kwa lengo la kushirikiana na wadau katika kumaliza tatizo la maji.
Amesema kuna haja ya Wakala huo kurudi katika halmashauri ili kupata mahitaji halisi ya miradi ya maji kabla ya kupanga bajeti ya kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma.
“Mrudi kwenye Halmashauri kule chini wao ndio wanajua mahitaji halisi katika vijiji ili mnapopanga bajeti yenu ilenge katika maeneo yenye uhitaji, pia katika kila Wilaya hakikisheni kuna bwawa ambalo litaweza kuhudumia vijiji viwili vitatu” amesema Dkt Mahenge.
Aidha ameitaka RUWASA kuhakikisha inapita kijiji hadi kijiji ili kuona hali ya upatikanaji wa maji na mahitaji yake halisi ili kuingizwa katika mpango kazi wao katika bajeti ijayo ya Wakala huo.
Amesema kuna haja ya kuwa wabunifu sana na kuacha kufanyakazi kwa mazoea na katika malengo yao wahakikishe kila kijiji kinapata maji na kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi ili huduma hiyo ipatikane kwa urahisi kwa wananchi.
” Lazima tuwe wabunifu kitengo cha ubunifu kiboreshwe kwani kwa sisi Mkoa wa Dodoma tuna maji sana chini ya ardhi na kipindi hiki cha mvua tunapoteza maji mengi sana tukiwa wabunifu haya maji yanayopotea yangesaidia sana” amesema.
Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Mkoa wa Dodoma Dkt Godfrey Mbabaye amesema lengo la kikao hicho ni kukutana na wadau na watumiaji wa maji katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma ili kushirikishana katika mipango waliyoiweka kuona kama inatija katika maeneo wanayotoka wadau hao.
Ambapo RUWASA imewasilisha mipango yao kupitia maada zilizowasilishwa katika kikao hicho amesema RUWASA wana jumla ya miradi 167 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na miradi 100 imekamilika sawa na asilimia 60.
Amesema hadi kufikia Desemba 2020 utoaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa vijijini ni asilimia 61.9 katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, amebainisha kuwa hadi kufikia mwezi juni 2021 hali ya upatikanaji wa maji itaongezeka hadi kufikia asilimia 67.2.
Ameongeza ” RUWASA Mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2020/2021 imetengewa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 9.3 na mpaka mwezi Desemba 2020 Mkoa ulipokea zaidi ya shilingi bilioni 4.1 sawa na asilimia 44.6 na kati ya miradi hiyo 25 ni mipya, 80 ni ya ukamilishaji na ukarabati na kukamilika kwake itaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 5.3.
Amebainisha kuwa katika bajeti ya 2021/2022 bajeti imelenga katika kutekeleza maagizo na maelekezo ya viongozi wa ngazi za kitaifa iliyotolewa katika maeneo husika, maeneo yasiyokuwa na huduma ya maji, miradi inayoendelea kujengwa, ukarabati wa miradi iliyopita mda wake au kuharibika na kupeleka maji katika huduma za kijamii.
Wakichangia maada katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Jabir Shekimweri amesema kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwani kuna miradi mingi imetengewa fedha nyingi lakini miradi hiyo haikamiliki na wananchi wanaendelea kulia kwa kukosa huduma ya maji.