WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akichimba Mtaro wa Maji Mtaa wa Kiruku Kata ya Mabokweni Jijini Tanga hivi karibuni wakati wa ziara yake ya siku moja
Picha ikionyesha Bwawa la Mabayani na Sehemu ya Mto Zigi ambalo ndio chanzo cha Maji Jijini Tanga
Picha inaonyesha Mradi wa Maji Muheza ambapo hilo ni tanki na kituo cha kusukuma maji kutoka eneo la Kilapura Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
Picha zinaonyesha eneo la mtambo wa kutibu maji Mowe
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Ujenzi wa Manhole Chamber kwenye Mradi wa Maji Taka wa Duga Mwembeni Jijini Tanga |
IKIWA ni siku chache kabla ya kuelekea maadhimisho ya wiki
ya Maji Duniani inayotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 16 hadi 22 mwaka huu hapa
nchini mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa imefanikiwa
kutekeleza miradi mikubwa sita ambayo itasaidia kuondosha tatizo la maji.
Hatua hiyo inatajwa kwamba itasaidia wananchi ambao walikuwa
wakikumbana na adha ya kusaka maji na kushindwa kujikita kwenye shughuli za
kimaendeleo kutokana na changamoto hiyo na hivyo kujikita kwenye uzalishaji na
shughuli za kila siku na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Miradi hiyo inatajwa kwamba itawawezesha pia kuongeza
uzalishaji wa huduma ya maji iliyokuwepo awali katika maeneo husika na hivyo
kupelekea huduma hiyo muhimu kwa jamii wa mijini na vijijini katika utekelezaji
wa shughuli zao za kila siku
Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii namna mamlaka hiyo
iliyojipanga Mhandisi wa Mipango na Ujenzi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Tanga Uwasa,Mhandisi Salum Ngumbi anasema ili kuhakikisha hayo yote
yanakwisha wamepanga kutekeleza miradi mikubwa sita kwa mwaka huu wa Fedha wa
kuboresha huduma ya maji Tanga kama ifuatavyo;
1.
Mradi wa kuboresha huduma ya maji Jijini Tanga
Awamu ya Pili (Phase II)
Anasema kwamba awamu hii ina lengo la kutaka kuongeza kiasi
cha maji kwenye Jiji la Tanga na wilaya ya Muheza ambapo kwa sasa mitambo yao
ya kutibu na kusafisha maji ina uwezo wa kusafisha na kutibu maji mita za ujazo
30,000 kwa siku hivyo mradi huo utaongeza uzalishaji wa maji kwenye vituo vyao
vya kutibu maji kutoka mita hizo za ujazo elfu 30000 kwa siku hadi kufikia
45,000 ambapo utakapomalizika utaondoa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanga
mjini na Muheza.
“Kwa maana hasa wakati wa mchana kuna kuwa na presha ndogo
ya maji kutokana na kuzalisha kiasi kidogo wakati Jiji la Tanga likiendelea
kukua kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali hivyo kuna ongezeko
la watu sana na sisi ndio wenye jukumu hilo na ndio maana tukabuni mradi huo”Alisema
Anasema waliamua kubuni mradi huo ili kuhakikisha wanakwenda
sambamba na azma ya Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha nchi inakuwa kwenye
uchumi wa Kati ambapo mradi huo utakuwa na gharama za Bilioni 8.4 ambao
unatekeleza na Tanga Uwasa kupitia fedha za Mkopo kutoka Benki ya TIB.
“Mradi huu utakuwa na kazi kama nne kubwa kukarabati mtambo
wa kutibu maji Mowe,miundombinu iliyopo ikiwemo kutanua mtambo na kuongeza
machujio mawili na clarifaya moja na hizo zote zitasababisha ongezeko la mita
za ujazo elfu 15000 kwa siku”Alisema
Mhandisi Salum anasema pia watajenga tenki jengine kubwa la
kuhifadhi Maji eneo la Mowe ambapo sasa hivi wana tenki la mita za ujazo 1,000,000
na watajenga jingine la pili lenye mita za ujazo 1,000,000 ili kukidhi mahitaji
ya maji eneo la mjini ikiwemo kujenga bomba kubwa lenye urefu wa kilimota 12.5 kutoka Mowe hadi eneo la Matenki Kange
Jeshini.
Anasema bomba hilo litakuwa na kipenyo cha Milimita 600 na hivi sasa wana bomba lengine lenye milimita
600 hivyo wanaongeza la pili ili kuhakikisha maji wanayosafishwa na kutibiwa
mowe yanawafikia wananchi kwa wakati
ambapo mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu na utakuwa na miezi 12
na utasimamia na wahandisi na wataalamu wengine kutoka Tanga.Uwasa .
2.
Mradi wa Uboreshaji Huduma Ya Maji Mji wa Muheza
Mhandisi Salum anaeleza pia mradi wa Pili utakuwa ni mradi
mkubwa utakao toa maji kutoka chanzo cha Mabayani na Mtambo wa kutibu Maji eneo
la Mowe na utamaliza tatizo la maji
Muheza kufikia asilimia 64 mradi huo utakuwa ni wa kuboresha huduma ya maji mji
wa Muheza ambapo utakapokamilika utasaidia kunufaisha wakazi wa Muheza 15,000
na wakazi wa Vijiji vya Jirani mradi huo unapopita.
“Maeneo hayo ni Kilapura ,Kitisa na Lusanga vitanufaika na
mradi huo ulianza mwaka 2019 na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 90 vitu
ambavyo vilipangwa kufanyika kwenye mradi huo ni kulaza bomba lenye urefu wa
kilomita 21.6 kutokea chanzo cha Maji Mowe hadi kwenye Kijiji cha
Kitisa”Anasema
Anasisitiza kwamba wataunganisha na bomba lililopo ambalo
likalofikisha maji mji wa Muheza kwenye Matenki ya NHC ambapo mradi huo
umeshaanza kutoa huduma hiyo kwa kutumia bomba lililopo la Pongwe na kwamba
wananchi wa Muheza wameunganishiwa kwa sababu kuna kipande cha kilomita 16.9 na
pia mradi huo ulihusisha ujenzi wa Tenki la Lita laki saba (700,000)kwenye
kijiji cha Kilapura na kituo cha kusukumia maji hivyo vyote vimeshakamilika na
vimeanza kutoa huduma.
Anaeleza kwamba kipande ambacho kilichobakia ni kulaza bomba
lenye urefu wa kilomita 8.2 na mpaka sasa wamekwisha kulaza kilomita 8 bado
mita 200 na wanategemea mpaka mwishomi mwa mwezi Machi mwaka huu utakuwa umekamilika.
“Lakini kwa hivi sasa tunatoa huduma na wananchi wa Muheza
wanapata maji kwa mgao kwa siku tatu kwa wiki Jumatatu,Jumatano na Ijumaa hivyo
mradi huo utakapokamilika wananchi watapata huduma siku saba kwa wiki na
kuondosha changamoto zilizopo “Anasema
3.
Mradi wa Kuendeleza Eneo la kutoa huduma ya maji
Jijini Tanga (Line Extension)
Hata hivyo anaongeza kwa upande wa Jiji la Tanga wananchi
wanaongezeka na kutanuka kutokana na wananchi wengi kujenga meneo ya pembezoni
mwa mji hatua ambayo iliyopelekea wao kuanzisha mradi ambao wana ufadhili wenyewe
Tanga Uwasa kwa gharamna ya shilingi milioni 320 wanatarajia kuongeza eneo la
utoaji wa huduma kwa kilomoita 20 mkwa mwaka huu wa fedha 2021.
Anaeleza kwamba mradi huo umekwisha kuanza na utawanufaisha
wananchi maeneo ya Kange Kasera Kange Mkurugenzi ,Pongwe,Neema,Mwakidila na
Masiwani,Mwahako na mafundi wao wapo kwenye maeneo ya mradi na wanaendelea kulaza
mabomba makubwa na wanatarajia kuwaunganisha
wateja wapatao 2000 mradi ambao wanautekeleza kupitia fedha za ndani ikiwemo kutumia
vijana wa mtaani kuchimba mtaro na mafundi wao.
4.
Mradi wa Kukarabati Mtandao wa Maji katika Mji
wa Pangani
Akizungumzia kuhusu wilaya ya Pangani,Mhandisi Salum anasema
wana mradi wa kuongeza eneo la utoaji wa huduma kilomita 15 ambapo wametenga
milioni 100 kwa ajili ya kufanya maboresho katika maeneo ya Boza,Mkalamo na
Madanga maeneo yote yatanufaika na mradi huo ambao unatekelezwa kupita fedha za
ndani watatumia wananchi na mafundi wao.
5.
Mradi wa Kukarabati na kuboresha Miundombinu ya
Maji katika Mji wa Muheza Awamu ya Kwanza (Phase I).
Akielezea namna walivyojipanga kuhusu uboreshaji wa huduma
ya maji Muheza kutoka asilimia 34 hadi 64 anaeleza baada ya kukabidhiwa
wamegundua miundombinu iliyokuwepo awali ni chakavu na baadhi ya maeneo mtandao
haujafika na waliandika andiko la kuboresha miundombinu mjini na walilipeleka
wizarani.
Anasema baada ya kulipeleka Wizara iliwaagiza wafanye haraka
watekeleze mradi huo na huo mradi una thamani ya Bilioni 4.8 lakini kwa awamu
ya kwanza wataanza na gharama ya milioni 500 mpaka sasa wanashukuru wizara ya maji tayari wamekwisha kupokea milioni 300 kwa
ajili ya kufanya ukarabati huo mradi na kuongeza eneo la kutolea huduma.
Mhandisi huyo anaeleza kwamba hivi sasa wapo kwenye hatua za
manunuzi ya mabomba na viungishio vyake wanatarajia watavipata mwishoni mwa
mwezi wa pili au mwanzoni mwa mwezi wa tatu hivyo watahakikisha wanakarabati
maeneo ambayo mabomba yake ni chakavu kwa kutumia fedha za ndani kwa saabu hivi
sasa wanapeleka maji kwa mgao.
“Lakini maji wengi yanamwagika mitaani kutokana na miundonbinu
mibovu watakarabati kwa kutumia wataalamu wao wa ndani na vijana kuchimba
mitaro na mradi huo utakamilika mwezi June mwaka huu na hivyo kuongeza wigo wa
upatikanaji wa huduma hiyo muhimu”Anasema Mhandisi huyo.
6.
Mradi wa Majitaka Duga Mwembeni
Kuhusu Mradi mwengine wa kuondoa maji taka na kuyapeleka
sehemu stahiki ambayo sio hatarishi
anasema wana mradi wa kujenga mradi wa majitaka kutoka eneo la Duga mwembeni
hadi katika kituo cha kusukumia majitaka kilichopo eneo lao la Makorora .