Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akibadilisha fimbo kutoka kwa Freddy Lukala ili kuweza kuupiga mpira kwenye muelekeo unaofaa wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameshika fimbo kuupiga mpira wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameupiga mpira wakati akifanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na mchezaji mwenzake Dkt. Aloyce Subhamilia na mara baada ya kufanya mazoezi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Gofu wa Gymkhana uliopo mkoani Morogoro kwa lengo la kukuza utalii kupitia michezo.
***************************
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wizara yake imeanza juhudi za kufungamanisha michezo na Utalii kwa maana ya Utalii wa Michezo ikiwemo ya Soka na Gofu
Amebainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati akifanya mazoezi ya gofu katik Uwanja Gymkhana Gofu Klabu uliopo mkoani Morogoro aliyoyafanya kwa muda wa siku nne asubuhi na jiono kwa lengo la kukuza utalii kupitia mchezo wa Gofu.
Hatua hiyo ya uhamasishaji ya kufanya mazoezi ya Gofu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amefanya wakati wa akifanya mikutano na Wadau wa Utalii iliyofanyika kwa muda wa siku nne mfululizo mkoani hapo.
Amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inaufanya mchezo wa Gofu kuwa kichochea cha kukuza utalii kwa kuandaa mashindano yatakayo wakutanisha watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia mikakati ya kukuza utalii wa michezo, Waziri Ndumbaro amesema ameiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Mikumi kuukarabati uwanja wa mpira wa miguu uliopo katikati ya Hifadhi hiyo ili timu mbalimbali ziweze kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mechi pamoja na kufanyia mazoezi ikiwemo timu ya Simba na Yanga.
Amesema kuukarabatiwa kwa uwanja huo kutasaidia kuongeza idadi ya Watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo ambapo amesema watu mbalimbali wakiwemo wachezaji na Mashabiki watakwenda kuangalia mechi wakat huo huo watapata fursa ya kuangalia makundi mbalimbali ya Wanyamapori wakiwa mbali kidogo ya uwanja wakiwemo nyati, simba pamoja twiga
Amesema katika nyakati za jioni Wanyamapori hao hupendelea kula chakula karibu na Uwanja huo, hivyo watazamaji wataweza kuufaidia
Amesema mbali na uwepo wa uwanja wa mpira wa miguu katika Hifadhi hiyo kuagiza ukarabatiwe, Pia ameagiza litafutwe eneo lingine katika Hifadhi kwa ajili ya kutengeneza uwanja wa kikapu hatua itayosaidia kuwavuta Mashabiki na Wachezaji wa mpira wa miguu kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Pia, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali inatarajia kufanya mashindano makubwa katika uwanja wa Gofu wa TPC Moshi kwa yatakayowakutanisha Wachezaji wakubwa wa mchezo huo wa kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuitangazia Dunia kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na ni sehemu pekee utakayoweza kuupanda Mlima huu na sio kwingineko.
Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameipongeza Klabu ya Simba kwa uamuzi wa kuwa Wazalendo kwa kuitumia nembo ya “Visit Tanzania” katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.