Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo (kushoto ), Naibu waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Ulega (ambaye alikuwa mgeni rasmi ), Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, na Mhifadhi Mazingira kutoka WWF, Dkt. Severin Kalonga wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa jumla wa kilomita 21 mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 Omary Maulidi (katikati ) , Rebecca Machege (kushoto ) na Grace Charles. Mbio hizo zilifanyika wilayani Kisarawe jana. Vodacom ilidhamini mbio hizo zenye lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi kupitia upandaji miti na utunzaji wa mazingira.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo, Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald wakishikilia utepe kabla ya kuanza kwa mbio za kilomita 21 za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 zilizofanyika wilayani Kisarawe.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo akibadilishana mawazo na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Mhifadhi Mazingira WWF, Severin Kalonga
Mshindi wa mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 kwa kilomita 21 wanaume, Omary Maulidi wa Dar es Salaam akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 1:12.
Washindi wa kilomita 10 mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo, Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Mhifadhi Mazingira WWF, Severin Kalonga
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo akimvisha medali mshindi wa kwanza wanawake kilomita 5, Assumpta Lameck