***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya polisi Tanzania licha ya kuongoza bao moja mpaka dakika 88 ya mchezo.
Fiston Abdulazak alianza kwa kuwatanguliza Yanga kwa bao alilofunga kwa umaridadi zaidi akipokea basi kutoka kwa Tuisla Kisinda kipinda cha kwanza cha mchezo.
Dakika 86 Mchezaji wa Polisi Tanzania Kelvin Yondan alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Fiston lakini haikuwazuia Polisi Tanzania kusawazisha bao dakika 89 ya mchezo.