Mwasisi wa Tuzo za Wanawake Bi. Fatuma Kange akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliondaliwa na Taasisi ya Raising Up Friendship Foundation.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation, Bi. Hilda Ngasa akizungumza katika Mdahalo wa Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
Baadhi ya washiriki wa mdahalo wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
……………………………………………………………………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Taasisi mbalimbali zinazopigania haki ya mwanamke wametakiwa kujipanga kwa kuandaa mikakati ya kitaifa ambao utamsaidia mwanamke kiuchumi.
Akizungmza leo jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani yaliondaliwa Taasisi ya Raising Up Friend ship Foundation kwa kushirkiana na wadau mbalimbali, Mwasisi wa Tuzo za Wanawake Bi. Fatuma Kange, amesmea kuwa ni vizuri taasisi kuwa na ajenda za kitaifa jambo ambalo litasaidia kupiga hatua.
Bi. Kange ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amesema kuwa familia nyingi kuna vilio, hivyo ni jukumu la kila mtu kuwa na mipango ambao utasaidia jamii kuwa salama.
“Tutengeneze miradi ya kitaifa ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu jambo ambalo litasaidia wanawake wanaingia katika sekta ya viwanda” amesema Bi. Kange.
Amefafanua kuwa maendelea bila pesa hauwezi kufanya kitu, hivyo inaitajika kuandaa mpango utakaosaidia kuleta ufanisi wenye tija.
Amesema kuwa miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja kuwa na utaratibu wa kuwaandaa watoto wa kike ili waje kuwa mama bora na kuleta taji kwa taifa.
Bi. Kange ameeleza kuwa ni jukumu la kila mwanamke kuwa kiongozi bora kuanzia ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation, Bi. Hilda Ngasa amesema kuwa miongoni mwa majukumu yao ni kuwasaidia watoto ili kuhakikisha wanakuwa na maadili ambayo ni rafiki kwa jamii.
Bi. Ngasa amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji majukumu yao ili kuziweka familia kuwa na maadili mema.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani wanawake, viongozi kutoka taasisi mbalimbali wamepata fursa ya kushiriki mdahalo wenye lengo la kuijenga jamii kimadili katika nyanja mbalimbali.
Machi 8 mwaka huu ni siku ya kimataifa ya wanawake, huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Wanawake katika uongozi: dunia yenye usawa.