Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga akiendesha kikao cha usuluhishi wa mgogoro kati ya Mmiliki wa Tamthilia ya Likuru the Village Elders Bw. Charles Ayuko (hayupo pichani) iliyoandaliwa na Kampuni ya Ladha ya Mtaa kutoka Kenya na Meneja wa Vipindi wa Televisheni ya Plus TV zamani Clouds Plus Tv Isaya Kandonga, leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam, baada ya kituo hicho cha televisheni ya Plus Tv kurusha Tamthilia hiyo bila kupata idhini ya miliki huyo na hii ni kutokana na kununua kazi hiyo kutoka kwa wakala tapeli na kuirusha bila kufanya uhakiki wa umiliki wa kazi hiyo.
Meneja wa Vipindi Televisheni ya Plus TV zamani Clouds Plus Tv Isaya Kandonga, leo Machi 06, 2021 Jijini Dar es Salaam akikiri kurusha Tamthilia ya Likuru the Village Elders bila kuhakiki vyema umiliki wa kazi hiyo baada ya kuuziwa na wakala tapeli aliyedai ni mmiliki wa kazi hiyo ambapo ameeleza uongozi wa Plus umeridhia kulipa milioni sita pamoja na gharama nyingine kwa mmlikili wa kazi hiyo Bw. Charles Ayuko kutoka nchini Kenya katika kikao cha usuluhishi wa kesi hiyo uliyoendeshwa na COSOTA katika ofisi zao.
Mmiliki wa Tamthilia ya Likuru the Village Elders Bw. Charles Ayuko (hayupo pichani) iliyoandaliwa na Kampuni ya Ladha ya Mtaa kutoka Kenya akitoa shukrani kwa uongozi wa COSOTA kwa namna walivyomsaidia kupata haki yake kwa maongezi ya amani baina ya pande zote mbili, baada ya Tamthilia yake kurushwa na Televisheni ya Plus Tv zamani Clouds Plus pasipo kuwa na makubaliano nae leo Machi 06, 2021, mara baada kikao cha usuluhishi kilichoendeshwa na COSOTA katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.