****************************************
NJOMBE
Wakulima wa Chai Tarafa ya Lupembe mkoani Njommbe Wamewataka Wawekezaji katika Zao la Chai kuwalipa madai yao ya mauzo ya chai katika Viwanda Vyao Ili kulinusuru Zao Hili liweze kuendelea Kustawi Zaidi katika Tarafa ya Lupembe Wilayani Njombe.
Rai hiyo imetolewa na Viongozi wa Wakulima Wa Zao Hilo akiwemo Neema Mbanga Kilian n walipofanya kikao cha Pamoja ili kujua Nini Mwafaka wa Malipo yao kutoka kwa Wawekezaji ambapo wanasema ni bora kuacha kuendelea na kilimo cha chai na kisha nguvu kuelekeza katika mazao mengine kama vile parachichi ,Mahindi ambayo hayatageuka mwiba katika maisha yao.
Wamesema wapo tayari kusitisha kuchuma majani ya chai na kuyauzia makampuni yaliyopo katika tarafa ya Lupembe kwa kuwa yamekuwa na usumbufu mkubwa pindi linapokuja suala la kulipa madai na stahiki za wakulima na wasafirishaji wa majani jambo linalovunja mioyo ya wakulima katika zao hilo la kimkakati nchini.
Awali akizungumza katika Kikao kilichokutanisha wakulima wa zao la chai katika tarafa ya Lupembe ambao kwa asilimia kubwa wako ndani ya mwavuli wa chama cha ushirika cha Mvyulu Mbunge wa Jimbo Hilo Edwin Ennos Swale mesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa mstari wa Mbele kuhamasisha Uwekezaji katika Viwanda ili Mazao ya Mkulima yapate Soko hivyo kuna kila sababu ya wawekezaji kuchukua hatua za haraka kulipa wakulima ili kuwa na ari ya kuwekeza zai katika sekta ya chai.
Swale amesema mgogoro na madai ya wakulima wa chai Lupembe una athari kubwa kwa uchumi wa Lupembe hivyo akiwa kama mwakilishi wa wananchi aliechaguliwa baada ya kuaminiwa anatahakikisha anaungana na wananchi kuitafuta haki yao katika kipindi chote.
Kituo hiki kimezungumza na mameneja wa kiwanda cha Ikanga Gerard Ngenzi na Alen Mbafu na Meneja wa kiwanda cha Igombora ambao wanaeleza sababu ya kushindwa kumaliza deni la wakulima kuwa na kuporomoka kwa soko la chai ulimwenguni na kusababisha chai nyingi kubaki gharani huku pia wakisema pamoja na changamoto hiyo wameendelea kupunguza madeni kwa kulipa kwa awamu huku madeni ya mwanzo yakipewa kipaumbele .