………………………………………………………………………..
Na Ahmed Mahmoud Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Happi ameitaka sekta ya Afya mkoani humo kuangalia namna nzuri ya kununua vifaa vya Afya ikiwemo MRI na Ct.scan hata kwa mkopo ili wananchi wapate huduma hiyo.
Happi ameyasema hayo kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo RCC kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha Mkwawa ambapo amewataka watendaji kuona namna nzuri ya kuondoa changamoto ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Alitoa ushauri kwa watendaji hao mkoani humo kuona umuhimu wa vifaa Tiba hivyo kuweza kusaidia kuondoa gharama kubwa kwa wananchi kufuata huduma hizo mikoa mwingine
Akawataka kuanza kujipanga upya na kuona umuhimu wa jambo hilo kuanzia kwa wabunge na watendaji Kuchukuwa agenda hiyo ya kuboresha huduma za Afya katika mkoa huo ikiwemo vifaa tiba hivyo kuona watasaidiana vipi kuboresha.
“Naona kuangalia upya suala la vifaa tiba ct.scan na MRI tutumie njia hata ya mkopo kutatua changamoto hiyo kwani inawezekana kuitatua na mkopo ukarudi baada ya wananchi kulipia huduma hizo”
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa amewataka IRUWASA kuangalia namna mpya ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwenye mkoa huo lengo likiwa utoaji bora wa huduma hiyo ndani ya manispaa ya Iringa na mkoa huo kwa ujumla.
Alisema kuwa huduma ya maji ni eneo muhimu sana ambalo inahitajika kuangalia kwa kina hususani uboreshaji wa vyanzo vya maji kwani ndio eneo muhimu linalosaidia uboreshaji wa huduma bora ya maji kwa mkoa wetu.
Alisema mkoa huo uwe na mpango mkakati wa kulinda vyanzo vya maji na mazingira kwa kuanza kampeni ya kupanda miti ndani ya mkoa kuongeza uoto wa Asili.
Cauption
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Happi akifuatilia usomaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwenye kikao cha Ushauri cha mkoa huo mapema leo kwenye ukumbi wa chuo cha Mkwawa mjini Iringa picha na Ahmed Mahmoud Iringa.
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha ushauri mkoa wa Iringa wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe hao mapema leo mjini Iringa picha zote na Ahmed Mahmoud Iringa