Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, Maulid Manu (kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mpwapwa, David Kinyage, wakati alipokuwa anawasili kituoni hapo kufanya ukaguzi wa utendaji kazi na pia kuzungumza na mahabusu waliopo kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Paul Sweya, baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Kibakwe, kilichofanyika katika ofisini kwa Mkurugenzi huyo, Mjini Mpwapwa, leo. Waziri huyo ndiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi Mpwapwa, David Kinyage, alipokuwa akimfafanulia jambo, baada ya Waziri huyo kukikagua kituo hicho pamoja na kuzungumza na mahabusu kituoni hapo, leo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, Maulid Manu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, Maulid Manu alipokuwa anatoa taarifa fupi ya kituo hicho kabla ya Waziri huyo kuanza kufanya ukaguzi wa kawaida pamoja na kuzungumza na mahabusu kituoni hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, baada ya kumaliza Kikao chao kilichofanyika Ofisi za Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa, leo. Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Paul Sweya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akitoka kukikagua Kituo cha Polisi Mpwapwa, na kuzungumza na Mahabusu waliopo kituoni hapo, leo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, Maulid Manu. Waziri huyo aliwataka askari na Maafisa wa Polisi wa Kituo hicho kuendelea kuwahudumia wananchi kwa haki.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimpa maelekezo Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa, Maulid Manu, baada ya kumaliza ziara yake ya kufanya ukaguzi wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya hiyo, Mjini Mpwapwa, leo. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.